Kisa cha serikali kuajiri wazee walio staafu na chama kuwateua wabunge viti maalum walio staafu

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Wana JF naomba kuuliza hivi kwanini serikali isiwape nafasi wanafunzi wengi wanao hitimu nafasi ya kujifunza kazi ili waweze kupata uzoefu wa kazi kwa masomo waliyosomea, ikumbukwe kuwa ni serikali tu ndio inaweza kutoa nafasi kwa sehem kubwa ya wanafunzi, na sio kwa sekta ya afya tu bali iwe kila mahali, nakumbuka nilienda kuomba EPZA wakasema hawana nafasi sasa sikujua sababu maalum, hii itatusaidia kuapata uzoefu katika kazi tulizo somea na itakuwa rahisi kuajiriwa sehem yoyote,

Nashauri kuwa serikali iangalie idadi inayo chukuliwa katika halmashauri na serikali kuu ni chache mno kila idara pawepo na watu kadhaa wanao jifunza kwa muda maalumu, mfano miezi 6 hadi 9 na badae kuwachukua wengine hii itasaidia sana.

Kuwapa nafasi ya kujifunza au kujipatia uzoefu wa kazi itasaidia kusitisha kuendelea kuajiri wazee ambao wamesha staafu maana hawa ndio wata replace nafasi zitakazokuwa zimebaki baada ya wengine kupandishwa vyeo na kujaza nafasi hizo, huu ni wakati mgumu sana kwa walio maliza vyuo hata kama hakuna incentives za kuwalipa basi wawape nafasi hivyo hivyo maana hata mimi ukinipa wazazi watanisaidia maana ni hazina.

Kuna kasoro tena kwenye kuwateua wabunge ambao wamesha staafu kurudia kuwa wabunge pamoja na kwamba kuna wanachama wengi ambao hawajawahi kuteuliwa pia ni watu sahihi kuteuliwa, hao wanao teuliwa sawa wengine unakuta wana watu wengi nyuma yao lakini si bado ni wanachama bado watu wako nyuma yao sasa haya maswala lazima serikali inayo jidai kuwa ni sikivu lazima iwe sikivu isiwe ni ya maneno tu.

Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wote wanao hitimu iwe priority kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi hao kwa baadae serikali inapo ajiri isiseme wenye uzoefu wakati haijachangia kwa sehem kubwa kuwapa wahitimu uzoefu, tumepoteza matumaini ya kuajiriwa na mashirika mana hatuna uzoefu wa kazi ukiomba serikalini wanakutolea nje lazima ma lazima uwe na ndugu ndio akuingize.

Rai yangu kwa serikali waongeze idadi ya wanao hitaji mafunzo kwa vitendo secta zote hata kama hamtawalipa, vyama viache kuwateua wabunge wastaafu kuwa wabunge.
 
Mbona hao vijana wamepewa nafasi awamu hii, wapo wengi tu mmoja wao ni mchapakazi Rc MH Paul Makonda
 
Nchi zilizoendelea hutumia sana hazina yao ya watu wenye umri mkubwa!! Uzoefu ni mwalimu muhimu sana na ndio maana CABINET ya serikali ya Maraekani imejaa watu wazima zaidi kuliko wakina Bashite!!
 
Back
Top Bottom