Kisa cha mwenye nyumba

Kisa cha mwenye nyumba

fired

Senior Member
Joined
Apr 4, 2021
Posts
184
Reaction score
394
Mimi ni mwanaume Nina miaka 36, nimeoa na tumejaaliwa kuzaa watoto watatu. Mwaka 2020 nilipata changamoto ya kikazi ilinipelekea kuyumba kimaisha, ivyo nikashindwa kulipa kodi, Sasa Kuna mama mmoja alikuja na kujifanya kama msamalia mwema, Kuna nyumba yake ambayo ilikua hazijaisha vizuri japo ilifaa kwa kuishi mana ujenzi uliobaki sio ule wa lazima. Akatuomba tuende kukaa kwenye hiyo nyumba nahisi alikua anatafuta mtu wa kulinda.

Basi tuliamia pale na mtoto mmoja, tukapata na wengine wawili. Sasa juzi kati ghafra tu mwenye nyumba akaja na kusema anataka afanyie ukarabati nyumba yake ili ahamie, akatupa miezi miwili tuhame, tukashtuka sana mana hatukujipanga kuhama kipindi hichi, Sasa kwanini alishindwa kutuambia mapema ili tujipange? yani kumlindia nyumba yake miaka mitano Leo hii anataka kutufukuza kama mmbwa, ama kweli shukrani ya punda ni mateke, tukijaribu kuongea nae atuongezee siku, anasema miezi miwili ni mingi na hapo amemuomba sana mume wake mana alitaka atugawie mwezi mmoja.

Hata ivyo sisi ni waungwana sana funzo mana Kunawatu hua wanawaroga wenye nyumba ili wasahau kama walijengaga, unakuta mtu analinda nyumba mpaka mwisho wa siku nyumba inakua kama yake, ila sisi hatukufanya ivyo, wema wetu ulituponza kumbe wanaofanyaga hivyo hua wanaona mbali sana.

Wamesababisha sasahivi naenda kuhamia ukweni, mpaka nijipate ni Leo? si nitakua nimesha oga dharau za Kila aina huko ukweni?
Sisi tumemuachia Mungu atatulipia kwa hili.

Angekua muungwana angetujengea hata chumba kimoja pembeni mana anauwanja mkubwa tu.
NAOMBA WAFIKISHIE UJUMBE HUU FUNZO
MANA WENYE TABIA HIZI NI WENGI HATA KWENYE NYUMBA ZA KUPANGA, WAPO WENYENYUMBA HUWAFANYIA HIVI WAPANGAJI WAO HII SIO HAKI.

Funzo media
 
Mda mwingne hata we jishtukie na uliandka hapa kweli ukae miaka 5 sehem bure afu unalalamika notice ya miez miwili. Wewe sema ulijisaha sa yamekukuta unabwabwaja bure cku hizi watu hawarogeki yaan kabla hujamroga yeye ashakuroga kitambo. Wewe hela zikakukosa za kulipa kodi had ukapewa bure yey atoe wapi za kukujengea chumba na kwanza akujengee kama nani kwa mfano. Tafuta mti mrefu upande juu kabsa afu ujiangushe kwa kutanguliza kichwa labda akili inaweza kurudi. Ucje kukubal kupewa nyumba uishi bure unajisahau wewe cha kutafuta n chakula tu no lipa nyumba ili uongeze limit yako ya utafutaji
 
Mtoa mada ana hoja asikilizwe,ishu sio kakaa muda gani pale,ishu ni notisi ya muda mfupi aliyopewa.

Kama angeambiwa labda kipindi cha miezi sita kabla na leo asingekuwa amejipanga hapo angekuwa amefeli,na kiukweli kabisa kwakuwa alikaa muda mrefu alipaswa hata apate taarifa mwaka mmoja kabla

Tusiwe wepesi wa kujaji mambo,hatujui kipato cha mtu kikoje
 
Kama miaka 5 ulishindwa kujipanga,ulitegemea mwenye nyumba akupe muda gani ili ndio ujipange?

Sijaona kosa la mwenye nyumba bali nimeona kosa lako wewe,

Wake up and get a life acha kutafuta huruma,Dunia ya leo haijalia watafuta huruma.
 
Mtoa mada ana hoja asikilizwe,ishu sio kakaa muda gani pale,ishu ni notisi ya muda mfupi aliyopewa.

Kama angeambiwa labda kipindi cha miezi sita kabla na leo asingekuwa amejipanga hapo angekuwa amefeli,na kiukweli kabisa kwakuwa alikaa muda mrefu alipaswa hata apate taarifa mwaka mmoja kabla

Tusiwe wepesi wa kujaji mambo,hatujui kipato cha mtu kikoje
...Notisi alikuwa nayo ya MIAKA MITANO, ndugu!
Toka alipoambiwa akae Bure pale, ilitegemewa yeye ajiandae kutoka kwenye hiyo dazo on day One!
Sio kusubiri upewe Notisi ya Miezi Miwili uanze kulalama! Usimdanganye, Ndugu !
 
Mtoa mada ana hoja asikilizwe,ishu sio kakaa muda gani pale,ishu ni notisi ya muda mfupi aliyopewa.

Kama angeambiwa labda kipindi cha miezi sita kabla na leo asingekuwa amejipanga hapo angekuwa amefeli,na kiukweli kabisa kwakuwa alikaa muda mrefu alipaswa hata apate taarifa mwaka mmoja kabla

Tusiwe wepesi wa kujaji mambo,hatujui kipato cha mtu kikoje
angepewa mwaka pia usingetosha mkuu.

haya mambo yaomeni hivi hivi. Nilimuachia dogo mmoja boda anikindie, wkt wa kuhitaji kuhamia akawa mgumu sana kutoka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom