Kisa cha Mwanamke wa ziwani - 3

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
KISA CHA MWANAMKE WA ZIWANI-SEHEMU YA MWISHO

Gordons Park na Carol enzi za uhai wao

Gordons Park

ILIPOISHIA……………..

Mahakama ilielezwa kwamba wanandoa hao hawakuwa na mahusiano mazuri katika maisha yao ya ndoa na kuwa walikuwa wakijihusisha na shajara za kubadilishana wanawake, maarufu kama ‘'wife-swapping' parties’ ambapo katika tukio moja la shajara ya chakula cha usiku Carol Park aliondoka na kwenda kulala na rafiki wa mumewe aitwae Colin Foster, huku Gordond Park akiondoka na mke wa Colin Foster kwenda kulala naye katika chumba kingine
ENDELEA KUSOMA HAPA……..

Lakini hata hivyo ushahidi wote uliokusanywa dhidi ya Gordons Park ulikuwa na utata mtupu kiasi cha kuwavutia watu wengi yakiwemo Makundi mbalimbali ya watetezi wakipiga kampeni ya kutaka Gordons Park aachiwe huru kutokana na ushahidi finyu dhidi yake.

Shahidi mwingine alikuwa ni mama mmoja aitwaye Joan Young, ambaye alidai kuwa mnamo Julai 1976 yeye na mumewe wakiwa katika mapumziko katika wilaya hiyo ya Lake walikuwa wamekaa kandoni mwa eneo hilo la Caniston na ndipo walipoona boti likiwa ufukweni.

Mama huyo alidai kumuona mwanaume akisukuma kitu kilichofungwa kama furushi, ambapo alimtania mumewe kwa kumwambia ‘yawezekana huyo akawa ni mkewe’
Hata hivyo ushshidi huo ulizua utata kwa sababu kwanza, siku na muda ulioelezwa ilitofautiana na ule uliokuwa ukifahamika na Polisi.

Pili, ingawa mumewe alikumbuka kusikia ule utani, lakini alikuwa akisoma gazeti hivyo hakuona kitu chochota. Tatu umbali walipokuwa wamekaa na umbali unaosemekana boti hilo kuwepo, ni vigumu kwa mtu kuweza kuona kitu na kukitambua.

Nne, kama aliona mtu akisukumia kitu ziwani, basi haiwezekani ukawa ni mwili wa Carol Park kwa sababu mwili ulipatikana umbali mrefu kutoka katika eneo ambalo wao Joan Young na mumewe walikaa. Ikumbukwe kwamba mwili ule ulikuwa umefungwa ndani ya begi la plastik pamoja na vyuma ili kuupa uzito usiweze kuelea, sasa itawezekana vipi kusogezwa umbali wote ule.

Tano, kwa mujibu wa maelezo yake wakati akifafanua kuhusu muonekano wa boti aliyoiona ufukweni siku hiyo alidai kuwa aliona boti la uvuvi kama Cruiser. Lakini wakati mwili wa Carol ulipopatikana ilifahamika kuwa Gordons Park alikuwa akimiliki Boti kubwa ya uvuvi aina ya Yatch.

Lakini mwaka 1976 Gordon alikuwa akimiliki Boti ieandayo kwa kasi ambayo ilikuwa ikitumika kwa uvuvi pia.

Ingawa kumbukumbu hazioneshi usahihi wa madai hayo lakini kuna ukweli kwamba Boti hiyo haikuwahi kuwepo katika ufukwe wa Caniston katika kipindi hicho cha mwezi wa tano wa summer, miezi miwili kabla ya Carol hajatoweka, kwani Boti hiyo ilikuwa ikitumika kuvua samaki katika ziwa jingine la Windermere.

Kama ikichukuliwa kuwa ni yeye aliyeutelekeza mwili wa Carol, basi mwili ule usingetelekezwa katika ziwa la Canistone na badala yake mwili ule ungetelekzwa mahali ambapo Boti la Gordons lilipokuwa ambapo ni Windermere, na kama ni kuogopa kuonekana na mwili ule na watu, basi angeenda maeneo ya mbali zaidi na sio Coniston mahali ambapo katika kipindi hicho cha Summer kunakuwa na watu wengi katika eneo hilo.

Mojawapo ya kidhibiti kilichofikishwa mahakamni hapo ni jiwe, ambapo mwendesha mashtaka alidai kuwa pamoja na kuutupa mwili wa Carol mtoni pia Gordons alizitupa nguo za Carol mtoni ambapo alizitosa zikiwa zimefungwa kama furushi na ndani yake kukiwa na lile jiwe.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa kitaalamu imethibitisha kwamba madini yaliyoko katika lile jiwe yanafanana kabisa na na madini yaliyoko kwenye mawe nyumbani kwa Gordons.

Lakini ni kwa nini mpaka jiwe likahusishwa na kesi hiyo? Hata hivyo katika hali ya kushangaza askari wa kikosi cha uzamiaji ambaye ndiye aliyehusika katika kuuopoa mwili wa Carol katika ziwa la Coniston alidai kuwa hakumbuki kuopoa jiwe hilo.

Naye Profesa Kenneth Pye ambaye ndiye aliyehusika na uchunguzi wa jiwe lile na akiwa ni shahidi wa kitaalamu katika kesi hiyo, alipoulizwa kuhusiana na mazingira ya kuhusishwa kwa jiwe hilo na kesi hiyo alidai kuwa ingawa ushahidi huo haukuwa na nguvu lakini ushahidi wa wale wafungwa wawili waliokuwa wamewekwa selo moja na Park wakati alipokuwa amewekwa rumande alipokamatwa kwa mara wa kwaza ndio muhimu katika kesi hiyo.

Ilielezwa mahakamni hapo kwamba mnamo Septemba 2000 mfungwa mmoja aitwae Michael Wainwright aliwasiliana na Polisi na kutoa taarifa kuwa Gordons Park aliwahi kukiri mbele yake akiwa na mwenzie aliyetajwa kwa jina la Glen Banks ambaye ana matatizo ya kutojua kusoma (Learning Disability) kuwa ni kweli alimuua mkewe.

Hata hivyo Park alidai kutokuwa na ukakika wa kukutana na watu hao alipokuwa gerezani.
Lakini Banks alionekana dhahiri kutokuwa na kumbukumbu nzuri wakati alipokuwa akitoa ushhidi wake pale mahakamani, kwani alisema, “Alituambia kuwa alimuua mkewe kwenye Boti huko Blackpool”
Naye Wainwright, katika maelezo yake wakati wa kutoa ushahidi mahakamni alinukuliwa akisema, “Park aliniambia kuwa alipopanda ghorofani katika chumba chao cha kulala alimkuta mkewe akiwa na mwanaume mwingine kitandani na ndipo alipomuua hapohapo”
Kauli hiyo ilizidi kuacha maswali nyuma, Je, ni nini kilichotokea kwa yule mwanaume aliyefumaniwa?

Lakini jambo lingine ambalo liliwashangaza watu ni hili, hivi inawezekana kweli mtu kama Park ambaye amekuwa mwalimu kwa muda mrefu na ambaye amekuwa akisisitiza kwa marafiki zake, familia yake, na hata mwanasheria wake kutokuwa na hatia tangu kukamatwa kwake kwa mara ya kwanza kwa kutuhumiwa kuhusikana mauaji ya mkewe, aweze kukiri kwa urahisi hivyo kwa watu hao ambapo mmoja wapo, yaani Wainwright, anahusishwa na uvutaji wa bangi kupindukia akiwa na uwezo wa kuvuta misokoto mpaka 12.

Na kama Gordons Park hakuhusika na mauaji ya mkewe, je ni nini kilichomtokea mkewe siku hiyo wakati walipomuacha mkewe nyumbani siku hiyo ya jumamosi Julai 1976?

Kulikuwa na mambo matatu muhimu ya kuyaangalia ambayo yalitokea siku hiyo. Kwanza jirani mmoja alimuona Carol akiwa amesimama nje ya nyumba yao, pili jirani mwingine alimuona mtu akiendesha gari dogo aina ya VW Beetle hadi jirani na nyumbani kwa Gordons Park na kusimama hapo kwa takribani dakika 20.

Tatu huyu jirani aliyeliona gari hilo aina ya VW Beetle alikuwa na uhakika aliyekuwa akiendesha gari hakuwa ni Gordons, ingawa hakumuona aliyekuwa akiendesha gari hilo, kwa kuwa aliliona likipita tu. Hata hivyo uwepo wa gari hilo katika eneo la tukio haukuwahi kuzungumziwa pale mahakamani.

Pamoja na utata huo, utata mwingine ni pale mwanamke mwingine ambaye alidai kumuona Carol majira ya jioni katika eneo la Charnock Richard services. Mwanamke huyo alisema kuwa alimuona Carol akikatiza mbele yake katika mwendo wa haraka lakini akiwa ameinamisha kichwa chini.

Katika ripoti moja kutoka kituo cha ushauri, ilionyesha kuwa tangu mwaka 1975 Carol hajawahi kulalamika kuwa amewahi kupigwa au kutishiwa maisha na Gordons kwa kipindi chote alichokuwa akihudhuria hapo katika kituo hicho.
Lakini hata hivyo miongoni mwa wapenzi wa Carol, wengi wao walikuwa na tabia ya ukatili na mmoja wapo alikuwa ni John Rapson ambaye ndiye aliyemuua dada yake na kufungwa gerezani.

Je Johna Rapton alikuwa gereani wakati Carol alipouawa? Hapana alikwishaachiwa tangu Disemba 1975, lakini alipohojiwa na polisi alidai kuwa alikuwa katika mji wa Barrow hapo mnamo Julai 1976, Carol alipotoweka.

Polisi hawakumtilia mashaka kuhusika na mauaji ya Carol, lakini wachunguzi wa masuala ya kiuhalifu walidai kuwa yeye John Rapton ni miongoni mwa wapenzi wa Carol wa kutiliwa mashaka kuhusika na mauaji hayo zaidi ya Gordons Park.

Kesi hiyo iliisha kusikilizwa hapo Januari 2005, ikiwa ni wiki 10 tangu ilipoanza kusikilizwa kwa mara ya pili, na ikiwa ni takribani miaka 29 tangu Carol alipotoweka.

Katika hali ya kushangaza Gordons Park alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kosa hilo. Lakini alipewa uwezekano wa kuachiwa baada ya kutumikia kifungo cha miaka 5 kama ataonyesha tabia nzuri.

Mnamo siku ya jumatatu januari 25, 2010, ikiwa ni imebakiza mwenzi mmoja, kufikiriwa kuachiwa, Gordon Park alikutwa akiwa amejinyonga katika selo yake huko katika Gereza la HMP Garth, Leyland, Lancs.
Je ni kwa nini achukue uamuzi huo wa kujinyonga wakati kulikuwa na uwezekano wa kuachiwa huru muda mfupi ujao? Hili swali mpaka leo halijapatiwa majibu. Kwa jinsi kesi hii ilivyojaa utata, na ndivyo hata kifo cha Gordons Park kule Gerezani kilivyojaa utata pia.

*****************MWISHO******************
 
ni nzuri lakini inasikitisha,pia imeshindwa kutufumbulia ukweli kuwa muuaji ni nani
 
Back
Top Bottom