Kisa cha Mfalme wa Wagagagigiko kutembea uchi

puza46b

Member
Nov 3, 2010
91
261
Hapo zamani za kale katika nchi ya Wagagagigikoko alikuwepo jamaa mmoja MASKINI lakini mwelevu sana aitwaye ABDUL(au tumuite Polepole!!). Siku moja aliketi chini na kutafakari kwa kina jinsi ya kuondokana na lindi la Umasikini. Mara, WAZO Pevu likamjia. Akajisemea moyoni, "nitakwenda Msituni na kujenga Kibanda kidogo. Ndani yake nitaweka Kiti kimoja na Viatu Pea MOJA". Kwa vile MFALME pamoja na RAIA wa nchi ya Wagagagigikoko walikuwa wamebobea kwa unafiki,uwongo, kupenda kusifiwa na kujipendekeza kwa MFALME, Abdul akajisemea mwenyewe, "nitatumia udhaifu wao kupata fedha.

Baada ya kumaliza ujenzi wa kibanda akaenda mjini na kuanza kusambaza uzushi ya kwamba alikwenda Polini, huko akakutana na MALAIKA aliyempa SIRI nyingi za MAISHA. Hata hivyo MALAIKA amesema kwamba MTU yeyote anayetaka kukutana na MALAIKA huyo sharti asiwe na DHAMBI. Kwamba MTU yeyote akiwa na DHAMBI hataweza kumwona MALAIKA, Bali ataona kiti na viatu tu. Watu wa Mji ule wakafurika kwenda kwenye msitu ule ili waweze kupata MAFUNUO ya MALAIKA. Kila alieingia KIBANDANI hakumwona MALAIKA Bali ni kiti kimoja Pamoja na viatu chini ya kiti kile... Hata hivyo kwa sababu ya HOFU ya kuonekana MDHAMBI, kila MTU alipotoka mlangoni Aliwamulia walio Nje UZURI wa MALAIKA na MAFUNUO aliyopewa...

HABARI za MUUJIZA huo FEKI ukawafikia MAWAZIRI hatimaye hata MFALME wa nchi ile ya Wagagagigikoko. Mawaziri wake wakamweleza juu ya Muujiza wa MALAIKA na Sharti la kumwona kwamba LAZIMA awe MTAKATIFU. Kwa madaha na MBWEMBWE Mfalme akapanda gari LA kukokotwa na FARASI na kufika hadi kwenye BANDA lile. Akavua viatu na kuingia ndani. Akachungulia kila kona bila kuona alama ya MALAIKA. Kutokana na AIBU ya kuonekana ni MDHAMBI mfalme akajitojeza nje na kuwatangazia RAIA wake UZURI wa MALAIKA yule FEKI na jinsi alivyopewa SIRI kubwa. Wakati Mfalme akiongea kwa Tambo kila aliyeingia mle kibandani akawa anajisemea moyoni nadhani Mimi peke yangu ni MDHAMBI maana sikumwona MALAIKA.

Baada ya Ujanja wa kwanza kufanikiwa ABDUL alimuendea mfalme wa Wagagagigikoko na UWONGO wa kupigia PESA.. Akamwambia anaweza kumshonea suti ya thamani sana ambayo wenye dhambi watakuwa hawaioni na wasio na dhambi tu ndio watakuwa wanaiona. Na kitambaa cha SUTI hiyo ni ZAWADI toka kwa MALAIKA..Mfalme akampa kazi Abdul ya kutengeneza suti ya aina hiyo kwa ajili yake. Kwa siku kadhaa Abdul alijifungia katika chumba akawa bize anashona suti ya mfalme. Baada ya siku tatu, mfalme akamtuma msaidizi wake akaangalie kazi inavyoendelea, yule msaidizi akaingia chumba alichokuwa akishonea Abduli lakini hakuona kitu japo alimuona Abdul akifanya vitendo kama vile yuko bize anashona nguo. Msaidizi akamwambia Abdul, ‘Nimetumwa na mfalme niulizie umefikia wapi?” Abdul akamjibu, “Kwani wewe huioni jinsi suti ilivyoanza kupendeza, ila bado namalizia nguo nyingine nataka kuanzia nguo za ndani ziwe ni hizi za kitambaa ambacho hakionekani kwa wenye dhambi”.

Hakika yule msaidizi alikuwa haoni kitu lakini ili aonekane hana dhambi akaanza kusifu jinsi nguo zilivyoshonwa kwa ufundi. Akatoka na kurudi kumueleza mfalme kuwa Abdul kamshonea nguo nzuri sana si za dunia hii kwa jinsi zilivyo nzuri. Mfalme alifurahi sana, kesho yake akamtuma msaidizi mwingine, nae kama yule wa jana akarudi kwa mfalme na ripoti nzuri sana ya maendeleo ya koti, pia akaleta taarifa nzuri kuwa kesho yake Abdul angemaliza kazi na angeleta nguo ili mfalme azivae. Kesho yake mapema Abdul akaingia katika kasri la mfalme akiwa kama kashika lundo la nguo, ambazo mwenyewe alisema wasio na dhambi tu ndio wataziona. Wasaidizi wa mfalme wote hawakuwa wanaona kitu lakini walianza kupiga makofi wakisifu jinsi nguo zilivyokuwa nzuri, hamna aliyekuwa anataka kuonekana ana dhambi.

Hatimaye Abdul akamkabidhi mfalme nguo, na kupewa KITITA CHA PESA.. Mfalme naye hakuwa anaona kitu lakini ili asiambiwe ana dhambi akajidai eti nae anaziona akaanza kumsifu Abdul kwa umahiri wake wa kuchanganya rangi na hata ufundi mkubwa wa kushona. Abdul akamuomba mfalme azivae zile nguo, wakaingia faragha mfalme akavua nguo zake na akaanza kuvaa nguo asizoziona kwa msaada wa Abdul. Kwa vile alivua nguo zote na kuvalishwa mpya zisizoonekana, rohoni mwake alikuwa anajiona yuko uchi lakini akaona akitangaza haoni kitu wananchi wangemshangaa kuwa mfalme ana dhambi, hivyo akaendelea kusifia na kujiangalia kwenye kioo akisifu nguo zilivyompendeza. Kisha akalazimika kutoka nje ili wananchi waone nguo mpya za mfalme.

Wote walikuwa wanamwona mfalme yuko uchi lakini wakawa wanaogopa kuonekana wana dhambi hivyo kila mtu akawa anashangilia na kusifu uzuri wa nguo za mfalme. Lakini ghafla mtoto moja mdogo (tumpe jina la TUNDU LISU) kwa sauti kubwa akamuuliza baba yake, “Baba mbona mfalme yuko uchi?”. Minong’ono ikaanza mwishowe watu wakaanza kumuunga mkono mtoto, mfalme aibu ikamshika kwani alijua sasa watu wote wanamuona uchi, akatimka na kujificha kwenye kasri lake na hadithi yangu imeishia hapo.
 
Hadithi nzuri. Rejea kitabu 'Oxford English Course book 5.' sisi tuliozaliwa mwaka 47 tunakumbuka, japo kuna mchanganyiko. Ile chapter yenye kichwa cha maneno 'Abdul's last trick' inaelezea hili.
 
Hahahahah kwa hiyo lile litoto litundu nalo lilikuwa uchi au?
Kwa nini linsingetulia siku ipite?
Hayo matoto malongo longo ndiyo yalipata laana kwa kuona uchi wa baba yao na kutangaza kwa mujibubwa bibilia.
🤣🤣🤣🤣
 
Hahahah kali sana hii..
 
Back
Top Bottom