Kisa cha mapenzi cha kusisimua

Kisa cha mapenzi cha kusisimua

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Habarini marafiki

Ni stori ambayo inasisimua na kushangaza na imeshatokea kwa wanandoa hawa
hebu marafiki isomeni najua hapa mtajifunza kitu toka katika STORY hii
Nimeinyaka mahali nami nimeona si vyema niwe pekee yangu nimeona nishare nanyi

MWANZO WA MAHUSIANO YAO YA KIMAPENZI







mume.jpg


Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.

"Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula,
nilimshika mkono na kumwambia, kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu
alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua
macho yake yalionyesha ana umizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza
kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno
yangu badala yake aliniuliza kwa sauté ya upole ‘kwa nini?' Sikumjibu Sali lake. Kutojibu
kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!' Usiku ule,
hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka
kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu?. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa Jibu
wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali, kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary.
Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwaMary. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba
yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu.
Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande. Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10
alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza
lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke
wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia.

Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu. Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa
majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika nakuwa jambo la hakika zaidi. Siku iliyofuata
nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani.
Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi
ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Mary.
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali Kabila nikajifunika vyema
shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote
kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa
kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote
mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana.

Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya
mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu
ya kuachana kwetu. Hili halikuwatatizo kwangu,nilikubali mango wake. Lakini alikuwa na sharti
la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu.
Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka
kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa.
Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.
Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga.
‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima', alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke
wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba
kwa mara ya kwanza sote tulinuniana.

Mwanetu alifurahi sana nakupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake'.
Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu
tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema
kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa
nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba. Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake
nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote.
Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya utur aliofukiza kwenye blauzi yake.
Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mkewangu kwa kipindi kirefu sana.
Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa
nyeupe!Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.
Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa
kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba
mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi
ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine
kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi. Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi.


Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa'.
Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi.
Ghafla jambo likanichoma... Mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake.
Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake.
Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini'.
Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mkewangu alimuonyesha
ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu
nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka
chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono Wake laini ulikuwa umeizunguka shingo
yangu kwa upendo. Nilimkumbatia Mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu.
Lakini wepesi wake ulinitia mashaka. Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata
kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu nakumwambia
sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini….
Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua...
.nikapanda ngazi. Mary alifungua mango nikamwambia, ‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu'.Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza‘Unaumwa?'
Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, kumtaliki mke wangu.
Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa
maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo
tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu,
nampenda mke wangu
sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.'Ikawa kama Mary alizinduka usingizini.
Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi
na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu.
Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu nakuandika
"Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kilo kitakapotutenganisha".
Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu Kuba usoni nikakimbia
mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani. Kumbe mke wangu
alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa
sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na
alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….
Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu...
Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira
ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na
mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako.
Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo
vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi
watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa
karibu wakati wa kujenga uhusiano wao.

Natumaini marafiki zangu mmweza kujifunza kitu hapa na kupata cha muhimu
kwenye mahusiano yenu ya ndoa au ya kifamilia pia.
 
Nshawahi kuisoma sehem. So nimefanya revision
 
inapendeza kukumbushana hata kama story ilishasomeka sehemu nyingine; Big up mtoa kamada.
 
Yani natamani kujua kilichopo lakini nimeshindwa kusoma.
naombeni summary wakuu.
 
Inamafundisho makubwa sana hii story
 
Dah! I've read this story 100! times(Not literally but u get the picture)! Yani kila nakoenda lazima niikute. Its really touching but are u not going to let it rest?
Mpaka mtaharibu maudhui ya kisa chenyewe
 
Tunakumbushana na kuna wengine hawajawahi isoma ina funzo kubwa sana
 
Nzuri sana ni tuisheni nzuri kwa wanandoa hasa waume.
 
Mimi ndo kwanza naiona na cha ajabu,Nime mkumbuka mke wangu ghafla.japo sina tatizo nae ila imetokea tuu kumkumbuka.Saa hizi nipo job.

wanao beza ni wale walio toolate kwa kina mary.
 
yaani ni stori nzuri sana,watu wengine wanaendekeza michepuko tu hawajali wake zao
 
Back
Top Bottom