Kisa cha kuelimisha

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
Binti mmoja alipita na gari yake, akamuona mzee mmoja akiuza mayai kando ya barabara. Akamuuliza 'Unauza bei gani?' Yule mzee akajibu "Tshs 250" kwa kila yai mjukuu wangu'

Yule binti akamwambia "mayai 6 utaniuzia kwa bei gani" yule mzee akasema "itakuwa 1,500 tu mjukuu". Yule binti akapandisha miwani yake nyeusi kwenye paji lake la uso kwa mikogo, kisha akasema " nitachukua mayai 6 kwa shilingi 1,000 vinginevyo naondoka.'

Mzee kwa unyonge akasema "chukua tu kwa bei unayotaka, Huenda ukawa mwanzo mzuri wa siku ya leo kwasababu tangu asubuhi sijauza yai hata moja".

Yule binti akalipa na kuondoka. Akaenda kwenye mgahawa uliokuwa jirani, na wenzake aliokuwa nao kwenye gari. Wakaagiza chakula cha mchana. Vyakula vilikuwa vingi. Wakala na kusaza. Vingi vilibaki juu ya meza kama makombo.

Muda wa kulipa ulipowadia mhudumu akaleta bill. Ilisomeka shilingi Elfu 45. Yule binti akatoa elfu 50 na kumwambia mhudumu "keep change"

Dakika chache baadae yule mzee alijisikia njaa, akaamua kwenda kwenye mgahawa huo uliokuwa jirani na alipokuwa akiuzia mayai yake, kuuliza kama anaweza kupata chakula cha shilingi 1000. Maana hiyo ndiyo pesa pekee aliyokuwa nayo. Lakini akajibiwa kuwa hakuna chakula cha pesa hiyo.

Kwa unyonge akaondoka. Kilichomsikitisha zaidi ni kuona yule binti aliyenunua mayai kwa bei ndogo amekula na kusaza kisha anasikia akimwambia mhudumu kuwa ile chenji inayobaki asiirudishe.

Maskini hukutana na changamoto nyingi wanapokuwa kwenye harakati za utafutaji. Tafadhali usiwaongezee changamoto. Jitahidi uwe sehemu ya kutatua changamoto zao.

Jiulize ni mara ngapi unapoingia kwenye maduka makubwa (Supermarkets or Shopping malls) unalipa Bei Ileile iliyoandikwa kwenye bidhaa husika, lakini unapopita magengeni Kununua mahitaji madogo ya nyumbani kama ndizi, nyanya, vitunguu, samaki, unaomba kupunguziwa Bei? Yani ndizi inauzwa Sh200 lakini unalazimisha uuziwe kwa Sh100.

Tafakari kuhusu huyu mzee na huyu binti, haya ndio maisha ya wengi wetu hasa ambao Mungu amewabariki kidogo. Leo unapo kula vyakula vya gharama na kutoka na familia yako "out" ni vizuri pia kujua kuwa wapo ambao hawana uwezo wa kupata hata mlo mmoja kwa siku.

Unapokuwa kwenye gari yako na ukahitaji kununua bidhaa yoyote kutoka kwa mchuuzi mdogo mtaani, using'ang'anie akupunguzie bei. Mlipe anachostahili na kama una ziada mpe pia. Mungu atakubariki.

Kwanini ulazimishe kuuziwa chungwa shilingi 100 wakati umeambiwa ni 200?? Unashusha kioo na kumwambia muuzaji kama hupunguzi sinunui, lakini unasahau shati lako ulinunua Mlimani City kwa shilingi elfu 50 na hukuomba upunguziwe.

Hii 200 ya muuza machungwa ina mzigo mkubwa wa mahitaji nyuma yake. Nyuma ya hilo beseni la machungwa kuna karo za watoto, pango la nyumba, nguo, chakula, matibabu etc. Usiwe sehemu ya kuwaongezea mzigo.

Aliyeruhusu wewe uwe katika nafasi unayoona ni nzuri kiuchumi, ndiye huyohuyo aliyeruhusu mwenzio kushinda juani akiuza mayai, machungwa, ndizi ili asomeshe wanae. Mheshimu, mthamini, mjali, muombee.

Mahatma Ghandi aliwahi kusema "If you cant help them, atleast dont hurt them". Yani "kama huwezi kuwasaidia, basi angalau jitahidi usiwaumize.!
SIKU NJEMA.
 
I don't know why, but really this message has struck me right off and changed my mood,,,
Ugh! This crazy world..
 
Ila jamani machinga tuna kazi

Mtu unamuuzia bidhaa 5000 hapo faida umepiga upate 2000
Ila mtu anakwambia nina 3000 kama hautaki basi,
Hapo unakuta haujauza siku nzima unasema ukubali urudishe msingi tu
 
Ujumbe mzuri,ukute ile 5000 ya keep change ndio mtaji mzima kwa babu wa mayai.Tuweni na moyo wakudaidia masikini na wahitaji.
 
Back
Top Bottom