SoC04 Kisa cha kijiji cha Mwendokasi

Tanzania Tuitakayo competition threads

JoJowin

New Member
May 2, 2024
1
0
Mwaka 2024 mwezi wa tano katika kijiji cha Mwendokasi, Kuna dokta mmoja anatokea kwenye chumba cha leba huyu anaitwa “dokta Steve”. Kwa mbele tunamuona mzee mmoja anakuja kwa haraka huku akiwa na wasiwasi anaitwa mzee “Sekwa”. Dokta anamtuliza na kumwambia mama kajifungua, mtoto yuko salama lakini mama kapoteza maisha kwa kupoteza damu nyingi sana wakati wa kujifungua.

Mzee sekwa analia sana na anaenda kukabidhiwa mtoto wake. Muuguzi anampa moyo na kumwambia “pole sana mzee mke wako kaagadunia lakini amakuachia zawadi ya mtoto wa kike”. Na hapo mzee Sekwa anampa jina mtoto wake la kisa, kisa sekwa.

Baada ya miaka 9 yani (2034) kisa amekuwa sasa na anaenda shule, shule ikombali sana na nyumbani. Inamlazimu kisa kuamka alfajiri na mapema iliawai shuleni. Siku za mvua kubwa kisa anashindwa kwenda shule, maji yamejaa sanaa barabarani hadi kwenye nyumba za watu ni hapa pitiki kabisa, miundombinu ni mibovu sana.

Shule anayosoma kisa inaitwa “shule ya msingi Mtakuja”, shule imechoka sana madawati Hakuna, vitabu vichache vya kufundishia, waalimu wachache na inasemekana waalimu wengi wamegoma kwa sababu hawaja lipwa mishahara yao. Kisa anaumizwa sana na hiyo hali na ukizingatia nyumbani ni mbali alafu anafika shuleni hapati huduma ya kufundishwa. Baba yake kisa ni mgonjwa anaumwa saratani ya koo.

Usiku mmoja mzee Sekwa anazidiwa, Kisa anajaribu kupiga kelele kuomba msaada. Anaenda kwa jirani mmoja hivi anaitwa mzee Yusufu, mzee Yusufu yuko na chombo cha usafiri yani (pikipiki) anatoka na kijana wake na kwenda kumsaidia kisa wampleke mzee sekwa hospitali.

Ile Wanafika njiani daraja linakatika katikati wanashindwa kupita, inawalazimu wazungukie kijiji kingine. Ile wanafika hospitali muuguzi anawaambia umeme unakatika katika hivyo wamuingize wampatie huduma ya kwanza huku wakisubiria

anampigia dokta bado mtandao unasumbua inabidi muuguzi atoke aende kumtafuta dokta njiani wanakutana na dokta, dokta anamwambia muuguzi “nakutafuta sikupati! twende kwenye chumba cha upasuaji kuna mgonjwa anasubiria huduma, tuwai maana umeme hauleweki” . Muuguzi naye anamwambia na mimi nimekufuata kuna mgonjwa anahitaji huduma dokta!. Yani hospitali nzima dokta ni mmoja tu!? kisa alijiuliza maana alimfuata muuguzi kwa nyuma .A

Mwaka unaofuata 2035 kisa anamiaka 11, ni mwaka wa uchaguzi katika nchi yao ya “Tanzanite”. viongozi mbali mbali wanapita kujinadi kwa sera zao na ahadi mbali mbali. kisa akiwa anatoka shuleni anasogea kumsikiliza mgombea mmoja wa kiti cha urahisi anaitwa mheshimiwa Nyota njema, yeye ni mgombea wa Chama cha Nuru (CCN).

Baada ya kujinadi anaomba mtu mmoja aulize swali. Wananchi wote wanabaki kushangaa tu hawana chakusema ni kama mgombea kawa fafanulia vizuri, lakini kisa kwa ujasiri wake ananyoosha mkono na kupewa nafasi. Anauliza maswali mazito sana, kwa umri wake ni vigumu kuelewa unaweza kusema alikaririshwa na mtu. Kisa anagusa Nyanja zote na sekta zote nchini.

Mgombea wa urais na waheshimiwa wengine wa serikali wanampigia makofi na watu wanamshangilia sana, Mheshimiwa Nyota Njema anainuka nakuanza kumjibu. Baada ya kumjibu anaomba akutane na kisa, baada ya kufungwa kwa mkutano kisa anakutana na mheshimiwa mgombea na mheshimiwa mgombea anamuambia nimevutiwa sana na kuguswa sana na maswali yako, tena katika umri mdogo sana.

Naona nuru kubwa sana inakuja katika taifa hili. Na mheshimiwa mgombea anamuambia kisa, omba mambo matatu na mimi ntakutimizia. Kisa bila uoga anamuomba mheshimiwa mgombea wa kiti cha uraisi. Kwanza amsaidie baba yake apate matibabu, pili amsomeshe hadi chuo kikuu, na tatu atakapo maliza elimu yake amuahidi kumpa nafasi ajiunge na chama hicho na agombee nafasi mbali mbali za uongozi. Bila kusita mheshimiwa Nyota njema ana muahidi kumtimizia hayo yote.

Miaka 15 Baadae.

Kisa amekuwa mkubwa sasa, na katika vipindi tofauti tofauti anasimamia miradi mbali mbali ya serikali bila shaka amekuwa mwanasiasa sasa. Anaweka saini ya mikataba mbalimbali ya uwekezaji na kampuni kutoka njee na ndani ya nchi hiyo.

Leo watu wengi wanamsindikiza wakiimba na kumshangilia “Nuru Nuru Nuru yale tuliyo yatarajia yametimia ……..”kisa yuko pamoja nao akilindwa kwa ulinzi mkali kweli bendera ya Chama cha (CCN) inapepea ni picha yake yenye sura ya furaha na matumaini ikipepea na kusindikizwa na ujumbe unaosomeka “hongera mheshimiwa raisi kisa msekwa Karibu nyumbani” bila shaka kisa amakuwa raisi sasa na yuko kwao kusalimia wananchi wake.

Kisa anaomba msafara usimame na mbele kuna bango kubwa pembeni ya barabara ya lami iliyo jengwa kwa viwango vya juu sana bango hilo lina pitisha maandishi ya ki electroniki yakisomeka “KARIBU JIJI LA MWENDO KASI”.

Kisa akasema ewe jiji la mwendo kasi umekomaaa sasa kiuchumi, elimu, miundombinu,afya na kadhalika unamchango mkubwa sana katika pato la taifa hili. Baadae kisa anakutana na wananchi na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa raisi wao na anawaambia “kwa sasa taifa letu liko katika uchumi wa juu vijana wanapata ajira, wawekezaji wa ndani na nje wameongezeka kwa salimia kubwa sana utalii wa nchi umeongezeka, kilimo kimekuwa ajira tosha kwa watu mbalimbali na hii ni kwasababu ya kutumia tekinolojia katika kilimo vijana wanapata ajira kwa wakati, matibabu ya kila aina yapo mikoa yote sasa afya ya baba mama na watoto wazee na watu wote inchini iko vizuri hospitali zipo kila kona elimu inatolewa kwa ubora wa hali ya juu. Usalama na ulinzi wa nchi yetu upo vizuri .

Hii ndio Mwendo kasi tuliokuwa tunaingojea na hii ndio Tanzanite tulio kuwa tunaitamani. Asanteni sana umeme. Muuguzi anamtafuta dokta mtandao wa simu unasumbua, mawasiliano hakuna, umeme unakuja na kukatika hiyo ndio hali halisi. Baaada ya muda fulani umeme unarudi vizuri sasa muuguzi.
 
Anauliza maswali mazito sana, kwa umri wake ni vigumu kuelewa unaweza kusema alikaririshwa na mtu. Kisa anagusa Nyanja zote na sekta zote nchini
Tungeyasikia na sisi hayo maswali na ufafanuzi wa mgombea mweeeh, tuwekee basi tuyasikie🙏

kwa sasa taifa letu liko katika uchumi wa juu vijana wanapata ajira, wawekezaji wa ndani na nje wameongezeka kwa salimia kubwa sana utalii wa nchi umeongezeka, kilimo kimekuwa ajira tosha kwa watu mbalimbali na hii ni kwasababu ya kutumia tekinolojia katika kilimo vijana wanapata ajira kwa wakati, matibabu ya kila aina yapo mikoa yote sasa afya ya baba mama na watoto wazee na watu wote inchini iko vizuri hospitali zipo kila kona elimu inatolewa kwa ubora wa hali ya juu. Usalama na ulinzi wa nchi yetu upo vizuri .
Ahsantee
 
Back
Top Bottom