Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Palikuwa na kijana mmoja aliekuwa na mpenzi wake, wapenzi hawa wawili walipendana sana. Walipendana mno kiasi kwamba hakuna mfano wa kuelezea juu ya upendo wao. Basi siku moja mwanaume alipata safari ya kwenda nchi za mbali, akafungasha mizigo yake na kuondoka.
Alipokuwa safarini mpenzi wake ambae alimuacha nyumbani ghafla alipatwa na ugonjwa wa ngozi. Akaharibika mwili wote, alijihisi vibaya sana maana aliwaza kwamba mpenzi wake akimuona hivyo anaweza akapunguza upendo sababu kaharibika na ugonjwa huo.
Zilipofikia nyakati, yule kijana alirudi kutoka safarini. Lakini hakurudi mzima alirudi na ugonjwa wa macho ugonjwa ambao ulimsababishia upofu. Basi mwenzi wake alipomuona karudi akiwa mpofu alifurahi sana kwa namna fulani maana alihisi penzi lao litadumu milele na milele kwani mapungufu yake ya kimwili (ugonjwa wa ngozi) mpenzi wake hatoyaona.
Kwa bahati mbaya siku moja, mwanamke huyo alidondoka ghafla na kufariki. Mpenzi wake alilia sana, baada ya mazishi jirani yake mmoja alimfuata na kumwambia "maisha yako yatakuwaje sasa ili hali u mpofu, na mwenzi wako ndio alikuwa akikupa huduma zote".
Mwanaume yule akavua miwani yake na kumwambia "Mimi sio mpofu, ila nilifanya hivyo makusudi ili tu kumtoa hofu mwenzi wangu ambae alikuwa akihisi nitamnyanyasa na kumtenga kutokana na ugonjwa wake. Asingekuwa huru tena kama zamani, ingempa ugumu sana kujikubali vile jinsi alivyo na ndio maana ilinibidi kujifanya kipofu niliyepata ugonjwa wa macho"
JIFUNZE: Kuna muda mbele ya baadhi ya mambo hatuna budi kujifanya vipofu kufumbia macho baadhi ya mapungufu ya wenzi wetu maana kamwe hakuna aliye mkamilifu. Si kila kitu tutaweza kupaza sauti zetu, mengine inabidi tuyafumbie macho na kuyamezea mate tu ili siku zizidi kusonga. Lengo ni kupendana na kudumu milele, na wala si kukosoana na kupiga makelele.
Ahsante kwa kunisikiliza naitwa [emoji2398] Amani Dimile