Kisa cha Jamaa Aliyemla mwizi wake

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,128
12,216
Habari wana JF

Juzi nilikuwa Morogoro katika harakati za utafutaji wa riziki, nilikuwa maeneo fulani nimejipumzisha mida ya jioni sasa pale nilipokuea nimekaa ni sehemu ambayo wanauza vinywaji, akaja jamaa mmoja akanisalimia ila hakuwa na uchangamfu kama ule tuliouzoea yaan ana uchangamfu wa kikauzu kauzu, akaagiza soda, alikuwa amekuja na baiskeli zile ndogo ndogo za swii swii, mimi nimetulia nashusha zangu kidang'a taratibu, kidogo simu ya yule blaza ikaita, akapokea sasa maongezi yake ndio kidogo yalinifanya niwe makini nae, alianza kwa kusema eeh unasemaje? ndio nishamnunulia mchele na viungo mpuuzi huyo, eeh wewe tulia nakuja mpika pilau kisha akatukana, akasema mkewangu kama wewe hautokula chinja jogoo hapo. Akakata simu.

Nikamuangalia yule jamaa, aah nikaendelea na yangu, sasa ndio akaanza nisemesha unajua kijana katika dunia hii kuna binaadamu wanataka tuwe wanyama? nikamuuliza kwa ki vipi brother? ndio akaanza kufunguka sasa! Anasema...

Yeye alikuwa anaishi Morogoro town miaka hiyo akiwa na familia yake, lakini kutokana na changamoto alizokutana nazo mjini ilibidi ahamie nje ya mji Mkundi huko sijui, na kilichomtoa mjini ni tabia za wizi, kwamba alikuwa na mkosi sana wa kuibiwa kwake, iwe kwa kuchaniwa wavu ama kuvunjiwa mara kadhaa, akaona isiwe kesi kwa kuwa alikuwa na pesa kidogo akaenda kutafuta shamba huko mkundi ndani ndani, akajenga ka kibanda akahamisha familia yake na mifugo yake, alikuwa anafuga kuku na hizo mjini ndio walikuwa wakimwibia sana,

Alipofika huko akawa pia anafyatua na tofali na kuchoma mkaa katika shamba lake na baadae mambo yakawa fresh kiasi akawa anapata riziki, anasema baada kama ya miezi 9 hivi kukaa huko, akagundua kuna mpuuzi huwa anaingilia mkaa wake shambani, yaani kuna mtu huwa anamuibia mkaa, jamaa ile kitu ilimuuma sana, akamuambia mkewe tumehama mjini kwa sababu ya kurudishwa nyuma sasa na huku pia? mimi nitamkomesha huyo mwizi na nitamuua mke akachukulia poa maana mmewe anamjua muoga na mpole, ooh ndio siku ya arobaini ya mwizi ikafika, jamaa anafika shamba live kamkuta kijana yuko na baskeli yake (ambayo ndio hiyo alikuwa nayo hapo muda huo anahadithia ). Kashapakia viroba viwili vya mkaa ndio yuko busy anamalizia cha tatu! akamvaa sasa huyo blaza ana mbavu, mwizi kidogo afya sio njema akazidiwa na yule blaza kauzu, akamtepesha kimya kimya huko shamba yaani ni mtu mbili tu, mpaka mwizi akatepeta kabisa.

Anasema alimweka begani akasepa nae mpaka lilipo tanuli anakochoma tofali, akatafuta kamba na mti mrefu akamfunga kama ndafu,( sijui ndafu anafungwaje mimi ) na baada ya kumfunga kama ndafu akaanza mchovya katika moto kule upande wa kichwa, anamuingiza, anamtoa, alirudia hivyo mpaka alipoona jamaa ameshakufa lakini aliendelea mpaka hasira zake zikaisha, sasa akawa anawaza akamtupe? akasema hapana huyu mimi NAMLA kwa maelezo yake yaani akimla ndio hasira zitaisha, basi akamkata miguu akaweka kwenye kiroba, akatoa kichwa na mikono, akamchana tumbo akatoa SWAINI ZOTE, dah mimi nikaona sasa leo nimekutana na jitu gani sijui, nilitamani niinuke nisepe lakini nikasema ngoja nimsikilize mpaka mwisho, anasema vile ambavyo alikuwa haitaji akaviweka katika kiroba akaenda kuvitupa mtoni, akarudi akachukua kile kipande yaan kutoka magotini mpaka shingo, akatia katika kiroba, kile kilichokuwa na mkaa nusu akamwaga akaweka mboga yake, akachukua na vile viroba viwili ambavyo mwizi wake alikuwa tayari ashapia ktk baskeli, akaweka na mboga yake juu akafunga vizuri, akapanda baiskeli mdogo mdogo anarudi kwake.

Kufika kwake mkewe akashangaa jamaa anarudi na baiskel tofauti na hayuko sawa yaani kama kawehuka hivi, akapaki akamwita mkewe ndani ndio akamuuliza mkewangu unajua kwanini tulihama mjini? mkewe akajibu sababu mjini tulikuwa tunarudishwa nyuma na wezi, akamwambia vizuri

Sasa mimi nimeacha raha zote za mjini nimekuja ishi huku shamba sababu ya hao swaini, bado wananifuata mpaka huku sada mimi leo nimemkuta mwizi ananiibia mkaa nimemuua na nimemkata vipande nimetupa na kingine nataka nimle, mke kusikia hivyo akataka akimbie akamwambia ukikimbia nitaanza na wewe au unapenda maisha haya tunayoishi? si unanipenda? badi wewe kaa zako kimya shughuri hii niachie mimi, akatoka akaenda kuiandaa mboga yake anasema alimbanika yule jamaa siku tatu ili atoke maji damu na mafuta na hiyo ndio ilikuwa siku ya tatu sasa kaja mjini na majogoo mawili kayauza na kanunua mchele kilo kumi na viungo anataka akampike pilau!.

Simu yangu ikaita nikashukuru sana, nikamwambia bro we sio mtu wa kawaida kwa heri mkuu! nikaenda zangu Msamvu nikachukua Bus kurudi Town!

Kweli kuna watu wamevurugwa dunia hii.
 
Mtakaosoma yote, mnipe summary/muhtasari.
Mtoa mada alikutana na jamaa mmoja. Sasa huyo jamaa akawa anamsimulia namna alivyomkamata mwizi wake wa mkaa na kuamua kumbanika kama anachoma ndafu kwenye tanuru la mkaa.

Mwizi alivyokufa jamaa akaona hasira hazijaisha anataka amle nyama ili hasira ziishe. Akampasua vizuri akambeba hadi home. Kufika home mke wake anataka kukimbia baada yakuona hayo, jamaa akamtishia piga kimya lasivyo nitakuua na wewe.

So jamaa akiwa anamhadithia mtoa mada, alienda town kununua mchele akapike pilau kwa kutumia nyama ya mwizi wake.
 
Kama ni kweli na anaenda akiropokaropoka hovyo kwa strangers hadi bar, muda si mrefu atajikuta nyuma ya nondo maisha!
 
Back
Top Bottom