Kirusi kinahofiwa kujitokeza Kwenye kompyuta leo

Kirusi kinahofiwa kujitokeza Kwenye kompyuta leo

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
96054399_cyberattack.jpg

Wataalmu wa usalama ya mitandao katika komputa, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine katika baadhi ya miji dunia, pale tu wataporudi makazini siku ya leo.

Inasadikika kuwa komputa zaidi ya 120 katika nchi kama 100, zilidukuliwa siku ya Ijumaa.Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya wanasema walioathirika ni 200,000 katika nchi 150.

Shambulio hilo limeathiri watumiaji wakiwemo ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, mabenki na huduma za afya.Hata hivyo kampuni ya Microsoft imesema kuwa tukio hilo ni kama funzo.

Taarifa kutoka kwa rais wa Microsoft na afisa mkuu wa maswala ya sheria Brad Smith siku ya Jumapili ilikosoa vile serikali zinavyoweka taarifa zao kuhusu dosari za kiusalama katika mifumo ya kompyuta.

‘Tumeona dosari zinazohifadhiwa na CIA zinaonekana katika Wikileaks na sasa dosari ilioibwa kutoka kwa NSA imeathiri wateja kote duniani’a ‘, aliandika Microsoft.

Kirusi hicho kilichojitokeza wiki iliyopita kiliweka dosari kwenye toleo la programu ya Microsoft Windows ambacho kilikuja kugunduliwa na majasusi wa Marekani.

Kwa sasa Kampuni nyingi zimeajiri wataalam waliofanya kazi wikendi kuzuia maambukizi mapya.Japo kuna hofu ya kirusi kipya kujitokeza siku ya leo.
 
Bora virusi vya Computer tutanunua nyingine kuliko virusi vya mwili. [emoji17]
Huwezi kujua umuhimu wa computer wakati umeijaza movie tu... Viwanda vikubwa kama vya bakhersa vinavyotumia mifumo ya computer ndio wanaelewa hasara kama hizi
 
Well, wewe ndio unasema hivyo, ila ungekuwepo huko ungejua hasa naongea nini..

Tembea uone.
Wakuu mbona mnashindwa kunielewa, computer sawa ina umuhimu na inahitaji kuwa protected
Ila huwezi compare computer life with you life.
Huwezi kujua umuhimu wa computer wakati umeijaza movie tu... Viwanda vikubwa kama vya bakhersa vinavyotumia mifumo ya computer ndio wanaelewa hasara kama hizi
Punguza mizuka ya movie, sasa huyo bakhresa akifa computer ikabaki so what next?
Alafu pia what matters the most ni data ambazo znaweza kuwa stored out from computer hata computer ikifa now, unaenda nunua nyingine na ku restore ?

Unaweza fanya backup ya maisha yako ukifa uji restore?
 
  • Thanks
Reactions: 247
Wakuu mbona mnashindwa kunielewa, computer sawa ina umuhimu na inahitaji kuwa protected
Ila huwezi compare computer life with you life.

Punguza mizuka ya movie, sasa huyo bakhresa akifa computer ikabaki so what next?
Alafu pia what matters the most ni data ambazo znaweza kuwa stored out from computer hata computer ikifa now, unaenda nunua nyingine na ku restore ?

Unaweza fanya backup ya maisha yako ukifa uji restore?
Hizo computers can kill people... Hujui kuna watu wapo ICU na kila kitu kinakuwa regulated na computer. Je ikifail huyo mtu hawezi kufa..?

Financial system ya dunia ipo kwenye computer, leo ukiambiwa benki yako ipo hacked si unaweza kupata pressure.

Hata utoaji wa dawa hospital unategemea computer, watu wanaweza kufa kwa kukosa important medication.

Miundombinu muhimu kama treni za umeme zinaendeshwa na computer.. hujui kama hizo computers zikifeli zitasababisha ajali?

Human life is beyond anything else.. but human life also depends on many things to prosper.. a short circuit in world systems which depend on computers may result in deadly consequences.
 
Hawa virus wanatambaa sana huyo anaitwa "Ransomware" pia kuna huyu IMG001 na KEY WANAZINGUA SANAAAA
 
Hizo computers can kill people... Hujui kuna watu wapo ICU na kila kitu kinakuwa regulated na computer. Je ikifail huyo mtu hawezi kufa..?

Financial system ya dunia ipo kwenye computer, leo ukiambiwa benki yako ipo hacked si unaweza kupata pressure.

Hata utoaji wa dawa hospital unategemea computer, watu wanaweza kufa kwa kukosa important medication.

Miundombinu muhimu kama treni za umeme zinaendeshwa na computer.. hujui kama hizo computers zikifeli zitasababisha ajali?

Human life is beyond anything else.. but human life also depends on many things to prosper.. a short circuit in world systems which depend on computers may result in deadly consequences.
Hawezi kukuelewa!!
 
Binadamu hawezi shindwa kuishi bila machine. Hizo computer ni msaada tu.
 
Back
Top Bottom