Kirusi cha mtwara kinazidi kusambaa

Kirusi cha mtwara kinazidi kusambaa

kigogo1ivi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
539
Reaction score
343
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Sekenke uliopo wilaya ya Iramba mkoani Singida wamesisitiza msimamo wao wa kutoondoka kwenye eneo hilo kumpisha mwekezaji mwenye leseni wala kutii amri ya mahakama inayowataka kusitisha shughuli zao.

Mahakama ya wilaya ya Iramba inayosikiliza shauri hilo juu ya mgogoro wa leseni ya madini baina mwekezaji John Bina na wenzake
na wachimbaji wadogo, imetoa amri ya kuzuia kuendelea kwa shughuli kwenye eneo lenye mgogoro hadi kesi ya msingi itakapo malizika.

Ni Kamanda wa polisi mkoa wa Singida kamishina msaidizi Linus Sinzumwa katika mkutano wake na wachimbaji wadogo wa dhahabu Sekenke akiwajulisha juu ya kuwepo kwa amri ya kuwaondoa lakini akaona vyema kukutana nao kuwasiliza kwanza kabla ya kutumia nguvu.

Hata hivyo baada ya kelele na zomea zomea ya muda mrefu hatimaye wachimbaji hao wakatulia na kueleza chanzo cha mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miezi sita hivi sasa.

Baada ya maelezo ya chanzo cha mgogoro,wachimbaji hao wakatoa msimao wao.

Licha ya mkutano huo kumalizika bila muafaka,jeshi la polisi limesisitiza juu ya utii wa sheria bila shuruti ili kudumisha amani na utulivu.

Inakadriwa kuwa zaidi ya wachimbaji wadogo 1000 wanaendesha shughuli zao kwenye eneo hilo lenye mgogoro katika mgodi wa
dhahabu Sekenke wilaya ya Iramba mkoani Singida.

SOURCE: Star tv
 
Haya tunataka msimamo wa Nchemba ili akitusaliti tutaanza na nyumba ya bibi yake Makunda na kumalizia na yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom