Kipindupindu kimekuwa donda ndugu Tanzania.Ugonjwa huu ambao ni rahisi sana kuuthibiti, kwa Watanzania inaonekana kama jambo lisilowekana kwa sababu ya lack of seriousness. Ninapotathmini mikakati ya wataalam wetu wa afya,nagundua kwamba yapo mapungufu mengi mno maeneo mengi.Kwa mfano, katika kijiji cha Wami Dakawa ambapo kwa sasa ugonjwa huu upo,mbinu zinazotumika kuuthibiti ugonjwa huu ni hafifu sana.Wataalam wa afya wahusika katika kijiji hiki sijui wamesomea wapi.Kulipaswa kuwe na "quarantine" inayosimamiwa vizuri ikizuia shughuli zote zinazosababisha mikusanyiko ya watu lakini hakuna hili halifanyiki kabisa.Mikusanyiko ya watu ipo na kwa ujumla shuhuli zinaendelea kama kawaida.Watu wanasafiri kama watakavyo na kufanya shughuli zao kama kawaida.Ipo Shule moja hapa ya Kata ambayo mpaka sasa wapo wanafunzi wawili ambao wamegundulika kwamba wana kipindupindu lakini masomo katika shule hiyo yanaendelea kama kawaida.Ni jambo la kushangaza kwamba hata katika hali hiyo,bado vyoo vya shule ni vichafu kupindukia.Sioni kama viongozi wa kijiji,diwani na uongozi wa wilaya kwa ujumla wanajibika ipasavyo.Nadhani kuna haja ya Mkuu wa Mkoa kulishuhulikia swala hili ili kunusuru maisha ya wana Dakawa.Kwa ujumla hili ni bomu linalosubiri kupasuka.Mazingira ya kijiji si rafiki hata kidogo.Vyoo Dakawa ni kitendawili.Sehemu zingine watu wanajisaidia hovyo hakuna vyoo kabisa.Hata wale wenye vyoo,vyoo vyao si salama kabisa,ni vichafu sana na vimejaa.
Naamini hali hii sio isolated to Wami Dakawa only.Ingekuwa vema kwa hiyo Rais akatoa tamko kwamba Mkuu wa Wilaya yeyote ambaye Wilaya yake itakutwa ina kipindupindu,ajiondoe mwenyewe,kwa kuwa nimeona uzembe wa wazi hapa Wami Dakawa.Nadhani hii itasidia watu kuwajibika inavyopaswa.
Naamini hali hii sio isolated to Wami Dakawa only.Ingekuwa vema kwa hiyo Rais akatoa tamko kwamba Mkuu wa Wilaya yeyote ambaye Wilaya yake itakutwa ina kipindupindu,ajiondoe mwenyewe,kwa kuwa nimeona uzembe wa wazi hapa Wami Dakawa.Nadhani hii itasidia watu kuwajibika inavyopaswa.