Kipindupindu chawaua watu 700 nchini Somalia

Kipindupindu chawaua watu 700 nchini Somalia

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
_96776360_6693671e-0e2e-4808-98a4-f1be597e0727.jpg
​

Watu zaidi 700 wamefariki kutoka na mlipuko wa kipindupindu nchini Somalia, kulingana na baraza la wakimbizi la Norway. Mlipuko huo unadaiwa kuwa miongoni mwa milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa huo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Baraza hilo limesema Sudan Kusini pia imeripoti visa visivyo vya kawaida vya ugonjwa huo.

Watu wengi haswa watoto wamefariki kutokana na kipindupindu zaidi ya vita nchini Somalia.

Sudan Kusini imerekodi vifo 160 kutokana na ugonjwa huo, ambao huwa nadra katika msimu huu wa kiangazi.

Hakukuripotiwa kisa chochote cha kipindupindu katika msimu kama huu mwaka jana.

Baraza hilo la wakimbizi la Norway limesema vita ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika nchi hizo mbili vimeharibu sekta ya afya na mfumo ya maji safi na maji taka.

Katibu mkuu wa shirika hilo, Jan Egeland amesema kuna hitaji la dharura la kupata maji safi, huduma za afya na dawa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Chanzo: BBC
 
Hicho kipindupindu kimeuwa watu wa ukoo gani huko Somalia? Nadhani kila ukoo utakuwa umeguswa na hilo janga. Tunajifunza kwamba wakati sisi tunabaguana kwa vigezo vya kijinga kama koo, dini, rangi, n.k. likija janga halibagui. Tuutazame ubinadamu wetu kuliko vigezo vya kijinga tunavyojiwekea ili kuhalalisha upuuzi wetu.
 
Dah poleni sana ndugu zetu wa africa kuweni makini huo ugonjwa ni wa kuambnkiza
 
Back
Top Bottom