Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Watangazaji wa kipindi cha Morning Magic cha Magic FM; OLES KAWAWA sijui KAWAO, KIBWANA DACHI , SALIM MKAMBALA NA MARY EDWARD ni WANAFIKI WAKUBWA. Kama hawako tayari kusikiliza serikali ikikosolewa basi wawe wanawaalika wale tu wanaowaona wana aina ya majibu wanayopenda kusikia. Kitendo cha kumuuliza maswali mgeni mwalikwa na kumtaka ajibu au atoe maelezo halafu wakati huo huo wanamzuia asijieleze, ni bora wasiwaarike wanaowaona au wanaodhani wanaikosoa serikali. Nawashauri wanapomuuliza swali mwalikwa katika kipindi chao ni busara wamsikilize mwanzo mwisho ndipo wamuulize swali au maswali. .Lakini kitendo cha kukatisha majibu au maelezo na kuchomekea maswali yenye mwelekeo wanaoutaka wao ni UNAFIKI. Kwami huwa wanalazimishwa kuchagua aina ya wageni wa kualika? Nawashauri ili waonekane POSITIVE au wafikiriwe ukuu wa wilaya wawe wanawaalika wageni wenye majibu wanayoyataka na unafiki wao..Sikupenda kabisa jinsi walivyokuwa wana mshambulia mgeni kwenye kipindic chao kwa maswali yaliyokuwa yanakatisha majibu au maelezo aliyokuwa akiyatoa. Busara ni kusikiliza kwanza kabla ya kujibu au kuhoji chochote