Kipindi hiki cha TBC 1 mlengwa ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi hiki cha TBC 1 mlengwa ni nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Apr 10, 2012.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kipindi cha "This week in Perspective" ni moja ya vipindi vizuri vyenye kuchambua mambo muhimu sana katika jamii ya kitanzania.Hujaribu kufafanua masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya jamii - kiuchumi, kisiasa na hata kijamii. Suala au mada huchambuliwa kwa kina na katika hilo hujaribu pia kugusia ufumbuzi wa baadhi ya changamoto zinazojitokeza.

  Mfano kipindi cha wiki hii kilikuwa juu ya "Youth and Employment". Mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na kuibua tatizo katika kutegemea ajira kwa vile kijana "kamesoma", kumbe basi kama mfumo ungeboreshwa, vijana wangeandaliwa mapema kabla hata hawajaingia vyuoni ili watakapofuzu mafunzo yao wajiajiri wenyewe.

  Kitu nilichoona ni kwamba mada zinahusu jamii za kitanzania.Nikabaki najiuliza, mada za kiingereza zitawafikiaje? Tunajua kabisa kwamba Tanzania inatumia Kiswahili kama lugha ya taifa, na isitoshe wasikilizaji wengi hawatumii lugha ya kiingereza. TBC ni TV ya taifa. Kipindi muhimu kama hiki hakiwezi kutafsiriwa kwa kuweka "sub titles",kama ni lazima kiingereza kitumike ili watu wengi wafuatilie.Au basi kipindi kiwe kwa kiswahili ili wananchi wafaidike na elimu inayotolewa kwenye kipindi hiki. Au walengwa ni akina nani?
   
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kipindi ni kizuri kama ulivyosema inawezekana kimewekwa makusudi pia kwa ajili ya kuwezesha wageni waalikwa wasiojua kiswahili pamoja na baadhi ya watanzania n.k wasiojua vizuri kiswahili waweze kutoa michango yao kwa ufasaha ila kingerushwa pia kwa Lugha ya kiswahili, mimi binafsi chambuzi zao fulani zilinisaidia sana kwenye mitihani yangu mwisho mwaka wa jana hivyo kwa wanachuo nafikiri kinamsaada.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kinatufikia jamani, hata kama kiingereza chetu ni cha kudokoa dokoa
   
Loading...