Kipindi cha pimp my ride kurushwa TZ wenye magari mkweche kaeni mkao wa kula

hawataweza,wataishia kupaka hayo magari gari lkn kuya-pimp kama pimp my ride ya marekani inavyofanya hiyo ni ndoto.
 
dah... Ebana mi ninao mkweche wangu kwa kweli unahitaji matengenezo ma nimebidi niupark kwa gharama za matengenezo..!!!
 
Wakina dada wamepinga vikali hiyo pimp my ride, wamesema wataunga mkono kwa wingi wakiletewa Pimp my body,hapo wateja watajazana sana.
 
Wakina dada wamepinga vikali hiyo pimp my ride, wamesema wataunga mkono kwa wingi wakiletewa Pimp my body,hapo wateja watajazana sana.

Kinadada wahusudu extreme makeover. Kubwa kuliko mkorogo na kukuza makalio.
 
Duh..Tanzania tutaacha lini copy n pest? We need to be creative. Inabidi tuje kitu chetu, siyo kukopi tu vya wenzetu kila siku.
Hii ilianza zamani sana .........toka tunaandika katiba yetu.. enzi zile... ushishangae
 
jana wameanza kurusha promo ya kipindi hicho wanadai lazima gari liwe na bima ya maisha
 
mikweche yetu ni zaidi ya mikweche, utakuta gari hadi filter holder imepigwa modification land cruiser inafungwa filter ya hiace, gear box gear zinachomoka za kushikiria, engine inachemsha, pad za brake hatununui mpya tunafanya bonding, mlango unafungwa na waya, vioo havipandi yaani kuripea gari moja tu na kipindi hakitarudiwa tena!
 

Ningechangia huu uzi lakini baada ya kuona hilo jina Clouds Tv basi tu! Ngoja nikalitendee tumbo langu haki kwakua sasa ni saa ya maakuli.
 

Mkuu nimecheka sana duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…