Kipindi cha "Mikingamo": Ujasiri huu umepotelea wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi cha "Mikingamo": Ujasiri huu umepotelea wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndyoko, Mar 17, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nikiwa nimepumzika nikiwaza hili na lile juu ya uovu wa CCM kwa nchi yetu TZ,
  na jinsi juhudi zinazochukuliwa na watawala ktk kushughulikia ufirauni wa CCM,
  ghafla nikajikuta nakikumbuka hiki kipindi ambacho pengine ni wachache tu wanaoweza
  kuwa wanakijua na kukikumbuka kwa jinsi kilivyokuwa mstari wa mbele
  kuweka hadharani uovu wa watawala wa wakati ule bila woga kupitia RTD.

  Najaribu kukumbuka maneno ya kibwagizo ya mtangazaji alokuwa akiendesha
  kipindi, 'TUAMBIE NANI, YUKO WAPI NA ANAFANYA NINI KUENDELEZA RUSHWA,
  ULANGUZI NA MAGENDO, NASI TUTAMTANGAZA HADHARANI...............hebu
  malizieni hayo maneno plz! Kwa anayemkumbuka mtangazi mahsusi wa kipindi
  kile anijuze please kwani nshamsahau! Nilikuwa nafurahishwa sana na lile
  tarumbeta la muziki ulokuwa ukiambatana na kipindi hiki............'

  Unayakumbuka haya maneno? 'Nikilala nikiamka aaaaaaaaah, mkaaaa hauonekani,
  'Sasa vita imetangazwaaa jamaaa, wananchi wote tuwe imara', vijijini na mijini
  tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi"............Aaaaaaaaaaaah, nchi imekwisha hiii
  imebaki longolongo tu, Mwl kaondoka na kila chake, umebaki uzushi tupu!

  J'mosi njema wakuu!

  My take: Kwa watawala tulionao hivi sasa hakuna ambaye anaweza kuthubutu
  kuanzisha na kukiendesha kipindi kama hiki kwa sasa na kukiendesha
  kwa namna kilivyokuwa kikiendeshwa miaka ile ya 80!
   
 2. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  ..Nasi tutamtangaza hewani na kwa wanaohusika.
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hiyo iliwezekana wakati wa mfumo wa chama kimoja.

   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kwa upande mwingine ilikuwa ni kipindi cha kupigia majungu na kujenga unafiki
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ilikua sauti ya Ahmed Kipozi, akisema, Mikingamo ni sauti ya umma, tuambie, yuko wapi na anafanya nini"... Duh!! Unanikumbusha mbali maana niliigiza kama 'Redio' nikiwa chini ya meza Maigizo Mawenzi Sekondari, Moshi.. Na sauti yangu nikimuigiza Kipozi, sikujua siku moja nitafanya naye kazi nikiwa katika fani moja na yeye. Kweli ilikua ni nguvu ya watawala. Wananchi na wanataaluma wa fani zote waliitikia wito, hata wasanii waliimba nyimbo za kuhamasisha mapambano dhidi ya rushwa! Umenifanya nitokwe machozi, nikiangalia jinsi rushwa ilivyogeuka kuwa kigezo muhimu katika kufanikisha mambo muhimu hata kuendesha siasa, uchumi na hata huduma! MUNGU INUSURU TANZANIA, Msaidie yeyote anayeitakia mema Tanzania yetu njema, Eee Mungu waangamize wanaoiangamiza Tanzania yetu njema kwa Ufisadi na Dhulma. Amin.
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hata humu kuna hayo unayoyaita 'majungu' lakini katika majungu 100 utakuta 75 yana data unazoweza kupata ukweli. Kazi ya umma ni kuleta hayo 'majungu' na dola ni kuyafanyia kazi kwa HAKI na kukusanya ushahidi. Leo mtu anaambiwa alete ushahidi, raia mwema atapata wapi ushahidi wa kimahakama? Leo Chadema wanaambiwa wapeleke ushahidi wa rushwa Arumeru uliompitisha Siyoi lakini rushwa iliyoshindwa kumpitisha Sarakikya na wenzake, badala ya dola kuwasilisha ushahidi husika ama kuwafikisha wahusika mahakamani. Hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu.
   
 7. T

  Tewe JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Duh mkuu ama kweli imekuuma hadi unakumbuka mikingamo! Uwapi uzalendo wa mikingamo hii leo kwenye vyombo vyetu vya habari?
  Tutamkumbuka baba wa taifa daima milele
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  how mkuu! hebu elezea mkuu
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135

  Umenikumbusha mbali sana Mkuu, Kila zama na kitabu chake! Mikingamo ilifanya kazi wakati ule, ... miaka ya 1983, sasa hivi tunayo JF inafanya kazi zaidi ya Mikingamo! wakati ule Mikingamo waliwashughulikia maafisa wadogowadogo wasingemgusa Waziri au kigogo yeyote (wakti ule tukiwaita VINGUNGE), leo hii utakubalina nami kuwa wale wahanga wa Richmonduli, EPA, etc. mawe yaliyowatungua yametokea humu JF.

  RTD's Mikingamo came and left us with same problems, JF will live forever!
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  aisee kumbe tuko wengi humu ndani tunaokumbuka mambo ya wakati uleeeeeee!
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  kidubwashika cha 'like' hakionekani kaka, u have said it all!
   
 12. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jamaa kanikumbusha mbali sana. Tena kilikuwa kila siku ya j5. Hivi hiyo sauti ilikuwa ya Kipozi au Salim Mbonde? Wimbo wa kuanzia kipindi ulikuwa.....Chama chama kimetukomboa chama * 2... Watanzania, wanamapinduzi, ni CCM yajenga nchi..Hapo redio ya mbao 88 3band inatema cheche ile mbaya.
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu umenikumbusha mbali sana....

  Unakukumbuka wimbo(jingle) wa kipindi cha Mikingamo?....

  'Bomu limeshapasuka Mabepari wanahangaika, wahujumu wanatapatapa........Walanguzi nao wako ndai eeee'

  'Nilikuwa mimi silali nikihangaishwa na mawazo.........Sababu ya hao walanguzi eee'

  'Nikilala nikiamkaa.....Sukari haionekani'

  'Nikilala nikiamkaa.......Sabuni haionekani'

  'Nikilala nikiamka aaaaa......Mfauta hayaonekani'...

  'Kumbe sababu ya walanguzi eeeeeee'.................

  Aisee...........
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kule Znz kulikuja kipindi cha Mawio kiliendeshwa na Marine Hassan na baadae wengine, lakini kilizimwa kiana!! Shamsi Vuai akiwa Waziri Kiongozi alikitetea lakini akazidiwa nguvu. Lakini, pamoja na kuwa zama hizo walishughulikia dagaa, mfumo uliokuwapo uliwashughulikia hao 'vingunge' na Mwalimu Nyerere aliwaminya kweli kweli na wengine hadi leo wanajitutumia na laana ya Malimu, hadi tunagundua tena na mapya huko Arumeru kutoka kwa Steve.... Yetu Macho, tuendeleze Mikingamo yetu hapa JF
   
 15. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  We acha tu, mtoto anaenda shule anasema anataka kuwa "Fisadi" maana mafisadi ni watu wanaobebwa juu juu kwa mbeleko ya kodi zetu na wapiga filimbi wanabanwa.
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Mtu wangu wa karibu alipakaziwa na kuishia kupata usumbufu usio na tija
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Tukumbuke enzi hizo chama kilikuwa kimeshika hatamu
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Halisi, William Sarakikya ana uhusiano na Gen. Sarakikya? Maana rushwa kweli ipo ila kwa leo hii haya maandishi yanafanya kazi kubwa sana kuliko "mikingamo" ya miaka ile
   
 19. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenikumbusha mbali sana mkuu!
   
 20. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Ni majina tu yanafanana....Hawana uhuiano wowote...
   
Loading...