Kipindi cha Jahazi na Kibonde kuhusu usalama na umuhimu wa kujihami na ajali

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,153
Nimekaa nasikiliza kpindi cha jahazi jamani kwanza wakaanza na topic ya leo usalama na umuimu wa kujihami na ajali zisizo na faida,nikajiuliza zipi zenye faida
baada ya hapo akaanza kuelezea mapungufu ya polisi likiwemo swala la kupokea rushwa
na utoaji leseni kwa watu wasio na uwezo ..akaanza kuelezea swala la leseni anapopewa mlemavu
wale wanaotoa wanamtakia nini ...akaeleza mengi ikiwemo leseni za kuendesha daldala wanaendesha
malori za magari madogo wanaendesha dala dala

mh kibonde akuishia hapo tu akasema anashangaa jeshi la polisi kusubiri mpaaka ajali itokee ndio
wanajitangaza kuimarisha ulinzi barabarani,akasema kwa nini mpaka mtu afe bana eeeh eehh na ameondoka huyu akishaulika kidogo tu wanaleegeza masharti mwendo wa kasikama kawa

akatuma msg mtu mmoja kuuliza kwa nini dadaetu aliachiwa ama kupewa leseni akusita kujibu nikweli na kama umenisikia nimeshangaa sana sana kwa nini na nani amemkabidhi na je ni mpaka afe mtu ndio wanajua mapungufu yao....

Ingawa ametoa pole baada ya kumaliza yaliyomo moyoni mwisho namshauri si vyema kuongelea amtu aliefika kwa babake alie juu kazi kwenu mlio hai mnaoshinda bar na kuacha familia zenu mwisho mnaacha gari bar mnakodisha tax kurudi nyumban
 
Sidhani kama kwa kusema hivyo anafurahia ajali...anahoji tu kuhusu ajali iliyotokea na aliyehusika katika ajali.
 
unamzungumzia bwana kibonde siku hizi ndo msemaji wa magamba kwenye hiyo radio
 
Kibonde is right hata kama mtachukia! Regia hakupaswa kuendesha gari mwenyewe! Mbona mtu akifa kwa ngoma mnaongelea sana humu? Double Standards!
 
Kibonde kilaza kweli kweli! Hii inaonyesha ni kiasi gani unaona kwamba walemavu hawana haki kama watu wengine. Mshukuru mungu wako aliyekuumba ukakamilika. Walemavu wanayo haki ya kuendesha kama wewe. Yapo magari maalum kwa ajili ya walemavu. Gari kama ni automatic mtu yeyote anaweza kuendesha. Ulemavu wa Regia unamruhusu kabisa kuendesha gari. Kibonde digest fikra zako kabla hujazungumza. Acha kumhukumu dada wa watu. Kibonde umekosa utu kabisa. Ajali ngapi zimetokea tangu kuzaliwa kwako? Zote ni walemavu walikuwa wanaendesha? Unaongea kama unajua kila kitu. Usihukumu nawe utahukumiwa.
 
jamani kibonde anamanisha kwa safair ndefu ni vizuri kuwa na msaidizi[dereva] kwa mtu TEGEMEO NA MPIGANAJI kama REGIA. Nadhani uongozi wa CHADEMA watafanyia kazi swala hili...x R.I.P REGIA.
 
Back
Top Bottom