Kipimo sahihi cha mafanikio yako

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
KIPIMO SAHIHI CHA MAFANIKIO YAKO:

Pamoja na changamoto nyingi zinazotuzuia kufikia mafanikio, kipimo nacho kimekuwa ni changamoto kubwa.

Kipimo unachotumia kwenye kupima mafanikio yako, kinaweza kukusukuma zaidi au kinaweza kukukatisha tamaa.

Aina za vipimo vya mafanikio.
Kuna aina mbili za vipimo vya mafanikio, moja inakusukuma kwenda mbele na nyingine inakukatisha tamaa.

AINA YA KWANZA
Kipimo cha umbali uliobaki wewe kufikia mafanikio yako. Yaani hapa unapima kile ambacho bado hujafanya. Kipimo hiki ndio ambacho wengi wanapenda kutumia na kimekuwa kinawarudisha wengi nyuma. Kama umepanga kufikia mafanikio makubwa, una mengi mbele yako ya kufanya, kadiri unavyofikiri yale ambayo hujafanya, ndivyo unavyoona bado ni magumu na makubwa.

AINA YA PILI
Kipimo cha umbali uliokwenda mpaka sasa. Yaani hapa unapima kile ambacho tayari umeshafanya mpaka sasa. Kipimo hiki kinatumika na wachache na kimekuwa kinawasukuma kwenda mbele zaidi. Kama umepanga kufikia mafanikio makubwa, kwa kuangalia yale ambayo umeshafanya tayari, unapata moyo kwamba hata yaliyopo mbele yako utayaweza.

Hali ni moja, lakini unavyoipima inaleta tofauti kubwa sana kwako na kwenye kufikia kile unachotaka.

Pima kile ambacho umeshafanya tayari na utasukumwa kwenda mbele zaidi. Pima kile ambacho bado hujafanya na itakuwa rahisi kwako kukata tamaa.
 
Sahihi kabisa.

Tunatakiwa kupima mafanikio kwa ambayo tumeyafanya.

Na tunatakiwa tupime kutokufanikiwa kwa ambayo hatujayafanya.

Ili ujipime kama una maisha mazuri lazima uangalie ambacho unacho.

Ili ujipime kama una maisha mabaya basi angalia ambacho hauna.

Mafanikio yanaendana na kumiliki.

Na kutokufanikiwa kunaendana na kukosa.

Na mafanikio ni kutimiza uliyoyakusudia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…