Kipi rahisi kwa serikali ya ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipi rahisi kwa serikali ya ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dopas, Jun 28, 2012.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Awali niseme tu pole kwa Dr. Ulimboka, mtetezi wa haki ya wanyonge:
  wa hospitali zetu na hata wa hali ya wafanyakazi ya idara ya afya.
  Inasikitisha kwa yaliyompata.

  Inasikitisha zaidi kuona kuna madokta wanafiki wanaendelea kujipendekeza kutoa huduma katika baadhi ya hospitali ili ionekane kuwa mgomo hauwahusu: ieleweke kuwa lengo la mgomo halikuwa tu maslahi ya madaktari, bali zaidi kuboresha hali ya mahospitali zetu.

  Najiuliza, sasa hao wanafiki wanaoendelea kujipendekeza wana malengo gani? Kama hakuna vifaa kwa magonjwa husika kwa hospitali kama muhimbili na nyingine zote, wao kuendeleza kimbelembele chao ni suluhisho? Labda kwa baadhi ya maradhi tu kama malaria, lakini kwa mengine yanayohitaji vifaa husika? Nadhani hili ndo hasa lengo la madaktari kugoma. Hili ndo alilosimimia shujaa Ulimboka. Mungu ampe ahueni. Na madaktari wazalendo wajitokeze kumhudumia huyu shujaa.

  Haya turudi kwenje swali.. tunasikia eti serikali imesema ....liwalo na liwe...liwalo na liwe lipi? Haya sasa limekuwa moja, Ulimboka kapigwa karibu kufa.. faida iliyopata hiyo serikali ya ccm kwa ujasusi huu ni ipi?
  Sisemi kuwa serikali ya ccm inahusika na ujasusi huu, ila kwa vile serikali ya ccm ina vyombo husika vya kuchunguza suala kama hili, nasema tu ituambie nani ni mhusika mbadala, kama sio wao ccm majasusi. Nipo tayari kutetea hili kwa viashiria vyao vya kijasusi.

  Pia tumesikia kuwa eti wana mpango wa kuajiri madokta toka nje ya tz(serikali ya ccm hao).... najiuliza swali tu.. kipi rahisi..
  kumwajiri dk kutoka nje? au kuboresha hali ya hospitali zetu na ya dokta mzawa? Je, Dokta kutoka nje ya tz atafanya kazi kwa miujiza wakati hospitali zetu hazina vifaa?... najiuliza tu maswali mengi bila majibu.. ingawa sishangai sana kuwa na serikali inayoamini zaidi miujiza kuliko vitendea kazi.. nasema hivi kwani nakumbuka wakati wa ishu ya babu wa loliondo tumeona jinsi walivyomiminikia huko kupata miujiza badala ya kuboresha huduma ya afya. Inasikitisha...............
   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kima hawezi kufanya upelelezi wa Ngedere kuiba mahindi wote ni jamii ya nyani.

  Ofisi ya Waziri mkuu na Ikulu zinahusika moja kwa moja na jaribio la kumuua Dr Ulimboka.
  Kwa umoja wao wa Kiibilisi walijua DR Ulimboka ni marehemu.
  Hili la kufanya upelelezi ni changa la macho kwetu wananchi.
  Tangu lini MiPorizi midogo inaweza kuichunguza MiPorizi mikubwa UWT??
  Hii itakuwa ni vita ya Mbwa na Fisi.

  Kama kawaida yao Ikulu na Ofisi ya waziri mkuu ya kuhudhuria misiba kwa mbwembwe za kijuha,Walisha anza kujiandaa kwenda msibani. Wasijue Mungu hana mshirika wala mwenza na hapangi mikakati yake na Bin Adam, sembuse binadamu dhaifu kama wao?

  Shock waliyopata baada ya kuambiwa Dr Ulimboka yuko hai was the biggest of all shocks, wengine kende zilinywea kwa juu kwa mfadhaiko.
  Waliokuwa wanavaa hirizi mbili viunoni mwao sasa wameshauriwa na vigagula wao wavae 13 kuondoa nuksi.
  Wengine wanawanga uchi wa mnyama na wakwe zao makaburini kuzuia zongo lisiwapate
  Some high ranked member of CCM government who strongly believe in witchcraft already are being haunted by this event and they know for sure some awful stuff are coming

  Mwishoni so likiwa zito sana wale jamaa walioshiriki kumpa kipigo Dr Ulimboka wote watageuzwa Kondoo wa Kafara ili kuzima soo. Ni rahisi kwa serikali ya CCM kuwaua wahusika wa jaribio la kumuua Dr Ulimboka kuliko kukabiriana na ukweli kwamba wana mikono yote miwili kwenye soo hili.
  Mmoja atanguka bafuni na kutoka mapovu mdomoni,
  mwingine ataumwa tumbo ghafla,
  mwingine atapa Cardiarc arrest,
  mwingine ataenda kulala kesho yake hataamka

  Hao ni CCM kigoda by all cost

  Si unajua tena, Uovu hauna kwao.
   
Loading...