Awali niseme tu pole kwa Dr. Ulimboka, mtetezi wa haki ya wanyonge:
wa hospitali zetu na hata wa hali ya wafanyakazi ya idara ya afya.
Inasikitisha kwa yaliyompata.
Inasikitisha zaidi kuona kuna madokta wanafiki wanaendelea kujipendekeza kutoa huduma katika baadhi ya hospitali ili ionekane kuwa mgomo hauwahusu: ieleweke kuwa lengo la mgomo halikuwa tu maslahi ya madaktari, bali zaidi kuboresha hali ya mahospitali zetu.
Najiuliza, sasa hao wanafiki wanaoendelea kujipendekeza wana malengo gani? Kama hakuna vifaa kwa magonjwa husika kwa hospitali kama muhimbili na nyingine zote, wao kuendeleza kimbelembele chao ni suluhisho? Labda kwa baadhi ya maradhi tu kama malaria, lakini kwa mengine yanayohitaji vifaa husika? Nadhani hili ndo hasa lengo la madaktari kugoma. Hili ndo alilosimimia shujaa Ulimboka. Mungu ampe ahueni. Na madaktari wazalendo wajitokeze kumhudumia huyu shujaa.
Haya turudi kwenje swali.. tunasikia eti serikali imesema ....liwalo na liwe...liwalo na liwe lipi? Haya sasa limekuwa moja, Ulimboka kapigwa karibu kufa.. faida iliyopata hiyo serikali ya ccm kwa ujasusi huu ni ipi?
Sisemi kuwa serikali ya ccm inahusika na ujasusi huu, ila kwa vile serikali ya ccm ina vyombo husika vya kuchunguza suala kama hili, nasema tu ituambie nani ni mhusika mbadala, kama sio wao ccm majasusi. Nipo tayari kutetea hili kwa viashiria vyao vya kijasusi.
Pia tumesikia kuwa eti wana mpango wa kuajiri madokta toka nje ya tz(serikali ya ccm hao).... najiuliza swali tu.. kipi rahisi..
kumwajiri dk kutoka nje? au kuboresha hali ya hospitali zetu na ya dokta mzawa? Je, Dokta kutoka nje ya tz atafanya kazi kwa miujiza wakati hospitali zetu hazina vifaa?... najiuliza tu maswali mengi bila majibu.. ingawa sishangai sana kuwa na serikali inayoamini zaidi miujiza kuliko vitendea kazi.. nasema hivi kwani nakumbuka wakati wa ishu ya babu wa loliondo tumeona jinsi walivyomiminikia huko kupata miujiza badala ya kuboresha huduma ya afya. Inasikitisha...............