yang
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 733
- 810
Nimekuwa nikijiuliza sana ni jambo gani kuu ambalo nikifanikiwa hapa duniani nitakuwa nimepata forever relief na kuleta maana ya kuwepo hapa duniani. Mimi binafsi bado sijapata jibu, naomba wadau tupeane maoni na ni kwa sababu zipi ukahisi jambo hilo ndio lenyewe. Hii nimefikiria sana sababu naona wengi tumejikuta tu duniani na tukaishi kama waliotangulia, na cycle ikawa moja kwa hii modern life yaani : kuzaliwa, kusoma kupata kazi, kuoa au kuolewa, kupata mtoto, kumlea mtoto hadi atakapohama kwako, kustaafu na kusubiria kufa. Hivi ndio umuhimu wa kuishi muda wote hapa duniani? Mbona wengine wanakufa na hawajafanya haya mambo? So kipi ni muhimu zaidi? Na kila mtu unakutana nae hata unaetamani uwe kama yeye anakuambia still anatafuta maisha. Ni lini maisha yanapatikana? Ni nini kuridhika na kupata haya maisha?
Msaada wa mawazo wadau.
Thanks
Msaada wa mawazo wadau.
Thanks