Kipi Muhimu kati ya cheti na transcript?

Kipi Muhimu kati ya cheti na transcript?

Livejr

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
2,073
Reaction score
2,812
Kip Muhimu zaid?

Kati ya chet cha chuo ambacho kinatolewa siku ya mahafali na Transcript ambayo inatoka muda mfupi baada ya mahafali?
 
Ktk dunia ya leo hasa kwa nchi kama Tanzania ambapo uzoefu na ujuzi havina kipaumbele, unalazimika kuwa na vitu vyote viwili yaani Cheti cha chuo pamoja na Transcript.

Ila kwa nchi za wenzetu linapokuja suala la kazi wanaangalia ujuzi kwanza kisha cheti baadaye ili kuhakiki na kuwekwa ktk ngazi au daraja sahihi la mshahara, wakati Tanzania tunaanza na undugu kisha Cheti kisha Transcript na hatimaye ujuzi utafuata kwa baadaye sana.

Muhimu kuwa na vyote hasa uwapo Tanzania.
 
Haya Maswali Yenye Majibu Halafu Yanaulizwa Huwa Yanakelaga Sana
 
Transcript ndo muhimu cause ni ngumu kufoji kupata transcript but vyeti watu wanafoji.
 
kila kitu kinaumuhimu wake ni vyema ukawa navyo vyote maana transcript ina onesha kila kozi uliyoisoma na ufaulu wake hivyo inaweza ikakuweka sokoni zaidi hasa km wanatafuta mtu aliyesoma kozi fulani. Lkn cheti nacho ni muhimu pia ndio maana unapewa hata km unatranscript na vyote havina expire date!
 
Vyote havina umuhimu wowote muhimu kuhifadhi modules ulizosoma kichwan mwako.
 
Vyote vina umuhimu na uzito tofauti. cheti hakioneshi matokeo yako ila uthibitisho/uhalali wa wewe kuhitimu sehemu fulani na huwa ktk hali ya origin. transcript inaonesha matokeo. Ktk aplication huwa vinaambatanishwa vyote.
 
Experience tu isiyopungua 10 yrs ndo ya muhimu.............. makazini watu hawana cheti wala transcript, we kaa navyo tu .............., ila uwe navyo mkuu
 
Vyote muhimu ila cheti huonyesha course ulosome na chuo husika. ila transcripit ni kuonyesha viwanga ulivyofauli kwenye course zako so vyote muhimu coz mfano penye ushindani wa kazi wote mwaweza kuwa second upper class

ila alama ikiwatofauti kwenye transcript huonyeshwi kwenye cheti so vyote muhimu km chungwa na ganda lake
 
Kuhifadhi modules!!!!????? ili iweje..?
na wewe unasapoti pumba??

Hizi pumba unazoziona hapa ni zile pumba zilizokobolewa na kuletwa hapa na mleta mada mimi nimezipepeta tu sababu tu kauliza pumba.
 
me naona transcript ni muhmu zaid ya chet,vyet vnafojiwa sana 2,ila transcript mfano za udsm unaanzaje kwanza kuzifoj,picha inakua scanned na inakua na seal ya chuo.
 
Back
Top Bottom