Si mara moja au mbili ni mara nyingi nimesikia kama si kwa viongozi waandamizi,basi viongozi wa dini.
Pia si haba kusikia watu wa kada mbalimbali nchini wakitoa wito wa kutunza amani.Vyombo vya dola navyo haviko nyuma katika kuwataka watu kuendelea kuitunza amani,sambamba na hilo wamekuwa wakiwatahadharisha wanchi kwamba vyombo vya dola havitaweza kumvumilia mtu yeyote atakayejaribu kuvunja amani. Pia jana ktk hotuba yake Rais amesema hatoweza kumvumilia mtu anayethubu kuivunja amani.
Swali langu ni hili hivi ni kipi kinachotakiwa kutetewa na kupewa kipaumbele kati ya amani na haki? Kwa ufahamu wangu naamini amani ni tunda linalozaliwa na haki. kutokana na andiko la Biblia Mithali 14:34 haki uinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.
Haki ndicho chanzo cha amani, Lakini sijasikia vyombo vya dola na viongozi waandamizi wakitetea haki kwa nguvu na kutahadharisha wale wote wanaowanyima watu haki zao kwamba wangekiona au kuchukuliwa hatua kali. Hivi ni kipi kinatangulia kati ya Haki na Amani?