Kipi kimekupita

Kipi kimekupita

Vyote lkn chandimu sitaisahau maishani mwangu. Nilicheza mpira vya kutosha.
 
Ukimuona zeru zeru unajitemea mate kwenye kitovu

mimi bibi yangu alinumbiaga hii inahusika zaidi na wasichana unatemea huku unasema Mungu niepushe niluvyoingia sec ndo nikaacha hii tabia baada ya kujua ukweli
 
Marufuku kumuonesha mwenzio kaburi/makaburi kwa kunyoosha kidole, et utakufa nawe.
daaah!

Mi mpk leo hii naifuatisha ati,bt mafindisho mengi yalikuwa ya kutishwa kama ukikalia kinu utaota majipu,ukilia kisu labda hata ndizi mbivu unaambiwa kitakata tumboni,wazamani tulilelewa vizur jaman tumekuja kujiharibu wenyew ukubwani
 
Kuendesha baiskeli ya miti kutoka kwenye mlima kuelekea bondeni
Timu yenye mpira uliotengenezwa na makaratasi akiona inapigwa bao kuweka mpira kwapani na kukimbia
 
Haya Mambo Huwezi Kuwa Umepitia kama Umezaliwa Baada ya Mwaka 90's...

1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana Kuvaa Nguo ya ndani aina moja nchi nzima VIP, usiombe ikakatika ukakuta imebana Kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bluce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kuisugua chini
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe zuri.
18. Ubitoz Ulikuwa ni Kusimamisha Kora Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".
20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakuambia "Utaipata Siku Ya Kufunga Shule".

Je wewe unakumbuka nini??
Hapa suala si miaka mkuu,bali ni hali halisi ya kipato cha familia uliyotokea.
 
Suala sio kipato Michael Jackson alikuwa anajuta kukataliwa kucheza na watoto wenzie hivyo akaamua kujenga neverland ukubwani, conclusion hakuna tajiri wala maskini kwenye michezo, nilikuwa natoroka na kwenda kucheza sana tu
 
Back
Top Bottom