Kumekuwepo na mijadala na majibizano mitandaoni kwamba kipi kianze kupatikana kati ya Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi.
Chama cha Chadema wao wanataka katiba mpya wakiamini ndio mwarobani wa changamito zinazoikabili nchi yetu.
ACT Wazalendo wao wanataka ianze tume huru ya uchaguzi kwanza ndio ije katiba Mpya.
Hoja yao ni kuwa bila tume, katiba mpya itasimamiwa na hii tume iliyoiba uchaguzi wa 2020 na hivyo kutoa majibu ya uongo kuhusu maoni ya wananchi.
Bila tume huru, kwenye kura ya maoni tunaweza kuambiwa wananchi hawataki mgombea huru, wananchi hawataki ukomo kwenye ubunge, yaani wanaweza kupindua meza huku wakiwa wammeshaandaa watu wa kufanya maandamano kupongeza.
Mimi binafsi naona tuanze kwanza na tume huru ya uchaguzi, ndipo katiba mpya ifuatie kukiwa tayari kuna refa mkweli.
Wewe unadhani kipi kianze?