Kipi kianze kati ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya?

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Kumekuwepo na mijadala na majibizano mitandaoni kwamba kipi kianze kupatikana kati ya Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi.
Chama cha Chadema wao wanataka katiba mpya wakiamini ndio mwarobani wa changamito zinazoikabili nchi yetu.

ACT Wazalendo wao wanataka ianze tume huru ya uchaguzi kwanza ndio ije katiba Mpya.

Hoja yao ni kuwa bila tume, katiba mpya itasimamiwa na hii tume iliyoiba uchaguzi wa 2020 na hivyo kutoa majibu ya uongo kuhusu maoni ya wananchi.

Bila tume huru, kwenye kura ya maoni tunaweza kuambiwa wananchi hawataki mgombea huru, wananchi hawataki ukomo kwenye ubunge, yaani wanaweza kupindua meza huku wakiwa wammeshaandaa watu wa kufanya maandamano kupongeza.

Mimi binafsi naona tuanze kwanza na tume huru ya uchaguzi, ndipo katiba mpya ifuatie kukiwa tayari kuna refa mkweli.

Wewe unadhani kipi kianze?
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya Panya kwa Mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu. Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa kuwa vinahusiana na chaguzi.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.
 
Naungana James Mbatia kuanzisha mchakato wa tume bila katiba Mpya ni sawa na mtoto kumzaa Mama
 
... kama kuna aliyemzaa mama yake yuko sahihi kupendelea ianze Tume ya Uchaguzi (ondoa neno huru maana ni hadaa za mchana kweupe) kabla ya Katiba Mpya.
 
Katiba kwanza, msisingizie Tume itahitajika kupitisha katiba no. Interim Tume could be appointed to pass the katiba then katiba izalize sasa Tume huru ya uchaguzi.
 
Kumekuwepo na mijadala na majibizano mitandaoni kwamba kipi kianze kupatikana kati ya Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi.
Chama cha Chadema wao wanataka katiba mpya wakiamini ndio mwarobani wa changamito zinazoikabili nchi yetu.

ACT Wazalendo wao wanataka ianze tume huru ya uchaguzi kwanza ndio ije katiba Mpya.

Hoja yao ni kuwa bila tume, katiba mpya itasimamiwa na hii tume iliyoiba uchaguzi wa 2020 na hivyo kutoa majibu ya uongo kuhusu maoni ya wananchi.

Bila tume huru, kwenye kura ya maoni tunaweza kuambiwa wananchi hawataki mgombea huru, wananchi hawataki ukomo kwenye ubunge, yaani wanaweza kupindua meza huku wakiwa wammeshaandaa watu wa kufanya maandamano kupongeza.

Mimi binafsi naona tuanze kwanza na tume huru ya uchaguzi, ndipo katiba mpya ifuatie kukiwa tayari kuna refa mkweli.

Wewe unadhani kipi kianze?
Wanasiasa watataka tume huru ya uchaguzi ili waingie madarakani lengo lao kuu,wapigania haki watatak katiba mpya yenye maslahi mapana kwa Taifa bila kujali ni serikali ipi iko madarakani
 
Wanasiasa watataka tume huru ya uchaguzi ili waingie madarakani lengo lao kuu,wapigania haki watatak katiba mpya yenye maslahi mapana kwa Taifa bila kujali ni serikali ipi iko madarakani
Nafikiri wapinzani waliobora ni wale wanaotaka Katiba ibadilishwe kwanza iwe katiba ya wananchi itakayo punguza madaraka ya Rais na nguvu hizo kupelekwa kwa wananchi na sio kukimbilia madarakani wakati katiba kandamizi ikiwepo. Naona wapinzani wanaotaka hili ndio wapinzani wanafikiria wanachi kabla ya masilahi yao ni wa kuunga mkono na sisi kama wananchi. Sio kuja na Cosmetic proposal za Tume kwanza katiba baadae. Vyama vinavyotaka hilo hawana mashiko. Tuondoe katiba mbovu kwanza Tume iwe zao la katiba hiyo ya wananchi.
 
Hakika umenena kiongozi ni lazima katiba mpya ipewe kipaumbele mengne yafuate👍👍
 
Wanasiasa wanatulaghai sana.
Kwanza wanasema Uchaguzi wa 2020 ni batili yaani Wabunge na Rais walishinda kimagumashi. Walienda mbali zaidi hata kudai kuwa hawaitambui serikali wakagoma kushiriki bunge wakasema hata wale covid 19 hawakuwateua.
Kwamba Bunge ni la KIJANI....

Hoja ni nini?

Kama Serikali na bunge ni haramu iweje tuwape hadhi ya kututungia katiba. Je katiba watakayoitunga itakuwa halali?
Katiba inatungwa na wawakilishi (halali) wa wananchi. Hili si Bunge halali na sio Rais halali mwenye political legitimacy Kwa sababu uchaguzi haukuwa huru. Bahati mbaya sana kwa sheria iliyopo Rais na Wabunge ni sehemu nyeti ya mchakato wa kutunga Katiba.

Sababu hii pekee inaonyesha ni lazima tuanze na Tume Huru tupate wawakilishi na Serikali halali yenye political legitimacy ili wasimamie na mchakato na hatimae kututungia Katiba Mpya.

Hoja ya Pili.
UWEZEKANO WA KUPATA KATIBA TUNAYOITAKA.
Kwanza ifahamike kuwa kupata katiba mpya ni mchakato wa Kisheria Kisiasa na Kidemokrasia ndio kusema mwisho ya yote kundi lenye MAJORITY ndio wataamua tuandike nini kwenye Katiba.
Kwa mujibu wa sheria ya kutunga Katiba bunge la katiba litakuwa na Wabunge wa aina 3
1. Wabunge wote wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
2. Wajumbe wa Baraza la wawakilishi wote
3. Wajumbe 210 kutoka vyama vya siasa na asasi za kiraia.
Ktk Wabunge 394 CCM sawa na 98%.. wapinzani ni 8 tukitoa wale kina Mdee waliofukuzwa kule Zenji kat ya Wawakilishi 77 upinzani wako 7 na 70 ni CCM sawa na 91%. Hawa 210, CCM inaweza kuinjinia upatkanaji ikawa at least 50-50..
Kwa nini nimeweka takwimu hizi. Ni kwa sababu kila kipengele cha katiba kinatakiwa kupigiwa kura na kipate 66% ili kiweze kuandikwa.
Je Wanaotaka katiba na wanataka vifungu wanavotaka viingizwe kwenye katiba wanaweza kupata hiyo 66% wakati upinzani wako chini ya 10%. Au ndio tuseme CCM watakisaliti chama chao waunge mkono Upinzani?
Kwa maelezo haya ni wazi hatuwezi kupata katiba Mpya bila kuongeza idadi ya wabunge wa Upinzani kuondoa udikteta wa Chama Tawala.
Ikumbukwe kwamba mwaka 2014 jaribio la kutunga Katiba lilikwama baada ya ya UKAWA kususa kwa kuwa CCM walitumia wingi wao kuandika Katiba watakavyo. Leo tuwaulize kama walishindwa wakati wanawabunge 100 leo wako 20 wataweza?

TUANZE NA TUME HURU
 
Hakika tunataka Katiba mpya tena I'll ya warioba. Japo kutakuwa na marekebisho ni kidogo Sana.

Katiba mpya ndiyo itaunda tume ya uchaguzi. Tume hiyo itafanya kazi kutokana na matakwa ya katiba hiyo.
 
Back
Top Bottom