General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,301
- 23,023
Uncle wangu ni Mstaafu na karibuni anategemea kupata mafao yake. Tangu katika utumishi wake hakuwahi kujenga na kumiliki nyumba. Fedha anayotegemea kupokea kwa makadirio ni 80M.
Wewe ushajenga ngapi mpaka sasa hivi? Ama kweli mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa!Kabla ya kumshauri naomba kwanza nimlaumu(samahan lakin)
1.Haingii akilini mpaka anafikisha Miaka 60 kazini Hajasimamisha ata chumba kimoja. Huu Ni uzembe wa Ali ya juu na haitakiwi kufumbiwa macho.
2.Kiinua mgongo hakiwekwa ili mtumishi akajenge, kile ni kwa ajili ya KULA TU matunda ya utumishi wake Miaka yote iyo aliyotumikia(kifuta jasho).
Maana yake ile ilitakiwa iwe pesa ya KULA mema ya nchi,utalii na vacation mbalimbali.
Ushauri:
1. Arudi Mkoani alikozaliwa akatafute Kiwanja Cha Bei nafuu, akajenge nyumba nafuu isiyozidi milioni 20-25
Kwanini nasema ivo: Akijitutumua kujenga hapa Mjini kwa mil. 60, atabakiwa na mil 20.
Sijajua ataifanyia nini ila Kama Ni kujiingiza katika utaftaji,
nakuapia atafeli vibaya mno maana purukushani za utaftaji kwa umri huo wa 60+ Ktk mji wetu huu hatoziweza kabisa, ATAKUFA KWA PRESHA BURE.
2. ASIWE NA WASHAURI WENGI WA FEDHA.
hapa wazee wa fursa washanusa mzee atashika mpunga mwingi mdA sio mrefu.
-Wazee wa MR. KUKU
(wekeza laki 7 upate milioni 70 kwa wiki 4)
-wazee wa FOREX
(wekeza Dola 1000 upate Dola 500,000 ndani ya nusu saa)
MSHAURI MZEE ARUDI BUSH ALIKOZALIWA, ALE MAISHA YAKE YALIOBAKI.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aliweza kupanga kwasababu alikuwa na ajira(kipato endelevu). Sasa hivi hana hicho kipato ana kiinua mgongo tu.Kama amestaafu tuseme ana miaka 60 hivi, anatarajia kuishi miaka mingapi mbele..? Jibu ni kwamba hatujui, tusimpangie.
Watoto wake tayari wanajitegemea, ni yeye na mkewe tu.... hiyo nyumba lengo lengo ni kumwachia nani..?
Aliweza kuishi kwa kupanga, alikotoka ni mbali kuliko aendako.... anaweza kumalizia safari yake bila ‘kumiliki’ nyumba.
Kuzika 60m kwa umri huo ni matumizi ya hovyo ya pesa, akule bata na mkewe na akiweza awasapoti watoto wake kama kuna sehemu wanahitaji ili safari ikiisha wamzike kwa heshima.
I moved your cheese, so what..!!
Ndo maana nimeomba samahani kabla sijamlaumu.Wewe ushajenga ngapi mpaka sasa hivi? Ama kweli mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa!
Naungana na huu ushauri. Washauri wote wa maswala ya kustaafu duniani wanakushauri ukishastaafu, kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhama mjini!!!Arudi bush , ajenge nyumba ndogo ya mil 20 hata kama ni chumba na sebure.. mil 60 atumie kuishi vizuri.
Mzee umefika 60 yrs hujajenga nyumba unategemea ujenge uzeeni ili aishi nani wkati watoto woote wanajitegemea..
Ajenge nyumba ndogo ya kumuhifadhi then ale maisha..
Btw pesa ya kiinua mgongo sio ya kujengea wala kununua gari (haya unatakiwa kuyafanya ujanani) hii ni pesa ya kukufanya ustaafu kwa amani bila kuwaza mambo ya chakula wala emergency ndogo ndogo.