Kipato duni kigezo cha kupata virusi vya Corona

Kipato duni kigezo cha kupata virusi vya Corona

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Watafiti wa Uingereza wamebaini kwamba watu wanaoishi katika mazingira duni nchini humo, wapo katika hatari zaidi kupata maambukizi ya COVID-19. Wakati, huko Brazil kumerekodiwa kiwango cha juu cha maambukizi.

Zaidi ya watu 307,000 wamekufa kwa COVID-19 duniani kote, wakati kumerekodiwa pia maambukizi milioni 4.5. Miji ya Ujerumani inajiandaa kuandamana dhidi ya vizuizi vya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona ambapo idadi kubwa ya watu inatarajiwa katika miji ya Munich, Berlin na Stuttgart.

Kwengineo watafiti wa Chuo Kikuu cha Oxford wamebaini kuwa kiwangio cha kipato ni kigezo muhimu katika kesi za maambukizi, ambapo wale wenye kipato kidogo wapo katika hatari zaidi ya maambukizi. Utafiti huo uliofanywa kwa watu 3,600 ulibaini pia wenye magonjwa sugu wameathiriwa vibaya.

Asilimia 29.5 wanaoishi katika mazingira duni walibainika kuwa na virusi ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya wanaoishi katika maeneo ya kitajiri. Watu wenye umri wa miaka kati ya 40 na 64 wamebainika kuwa katika hatari zaidi ya asilimia 18.5 ikilinganishwa na kundi la umri wa miaka 17 ambao wapo katika hatari ya asilimia 4.6.
 
Kina Mbowe walikuwa wanalilia lockdown Kwa sababu wana lipwa na serikali

Bora Rais Magufuli aliwashtukia wale masela
 
Hapo umedanganywa sana na tafiti za kipuuzi. Kule mbagala, Tandale, Mwananyamala, Gongo la Mboto, Buza, Msasani, Kinondoni , Buguruni Maiti zingetapakaa. Lakini mambo ni Ajabu kabisa gemu lipo Mbezi beach, Kunduchi, Oyster bay. Sasa amka waza sana. Corona siyo kipindupindu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom