Kipanya leo!!

Kipanya leo!!

Kipanya leo umechemka. Tanzania siyo soviet union au federal state, kwa hiyo disintegration ya namna hiyo haiwezi kutokea. Nenda uje vingine.

Mkuu angalia sana upokuwa unakosoa katuni za huyu bwana. Kimanya is the smartest politicatoonist the country has ever had. Catoon moja ya Kipanya inaweza kubeba maudhui yote ya alichotaka kuonesha, hivyo yakupasa kufikiria sana ili kumuelewa huyu bwana.

Anaposema mikoa yote itataka kujitenga ana maana kubwa sana, kumbuka kauli ya Pinda 'kuwa Zanzibar si nchi' - maana yake kama si nchi ni mkoa au?, pia angalia mzozo ulioanzishwa na kauli ile huko nyumba na mlolongo wa matukio ya hivi karibuni. Katuni za Kipanya ni za kuziangalia na kutafsiri unavyojua wewe ila kuanza kuzikosoa utakuwa wewe ndiyo unachemsha
 
Mchaga hatojitoa labda malii sake mikoa yote sifidiwe na awe na passport saidi ya moja saa kurudi angalau kuwapa mbeke kidoko wasee walioalala chini.Na kutafuta wadoko zake manka kila mwaka.

Warangi ili mradi Arusha isiwe kambi tofauti na wao kwani ofa ya kuishi miskitini na majumbani kwa waAsia kunawafanya wajihisi kuwa karibu zaidi na imani yao..Ni Nkamia tuu tuu,ndio atapenda dar isiwe kambi tofauti.
 
Kachemka Kipanaya au character wake? BTW Tanga itakuwa ya kwanza kujitoa maana iliungana na Nyika (pori) kuunda Tanganyika....nyika imetokana na neno la kijerumani nieker maana yake pori


Mkuu hapa unaandika upya historia na kwa bahati mbaya unapotosha. Hata kama kuna neno la Kijerumani linalofanana na Nyika, ukweli ni kuwa hilo ni neno na asili la lugha nyingi za jirani zetu wa mkoani Tanga. Nyika kwao ni pori. Vijana Jazz waliwahi kuweka sawa jina la Tanganyika. Tanga kwa lugha za huko (pamoja na maana nyingine) ni shamba hasa la mbali na nyumbani (wengine huita "kutanga").
Inavyoelezwa ni kuwa Wajerumani walifika kijiji ambacho kinaitwa Tanganyika (njiani ukienda Tanga baada ya Muheza na kabla ya kituo cha utafiti wa kilimo Mlingano). Muda huo watu wazima walikuwa mashambani hivyo wakakuta watoto wadogo. Wakawauliza wazazi wao wameenda wapi watoto wale wakajibu "waita tanga" maana yake wameenda shambani. Basi Wazungu wale wakasubiri mpaka watu wazima waliporejea. Wakajifanya wao wazungu wanajua kuwa mahali pale panaitwa Tanga. Wakauliza kama hapa ni Tanga huko kwingine kunaitwa jina gani, wakajibiwa kuwa "uko n nyika". Maana yake huko ni pori. Ndipo Jerumani wale wakajua kuwa nchi yetu eti ina Tanga (yaani shamba) na nyika (yaani pori). Kwa kifupi hiyo ndivyo ilivyokuwa katika kupata jina Tanganyika. Ikiwa huridhishwi na maelezo haya waweza kufika kwenye kijiji kile cha Tanganyika ukajipatia ukweli wa kihistoria. Hivyo utajua maana ya jina la mtani wao (watu wa Tanga), mbunge wa Ubungo. Kuna mpaka methali za neno mnyika. Wasambaa wana usemi kuwa "Mnyika n ngogwe heeka kashungu". Ikiwa na maana kuwa "mtu wa porini (kusikojulikana) ni sawa na nyana chungu, haachi uchungu (au kuwa mchungu). Hakuna nyana chungu isiyo na chungu. Hivyo ukiona Mnyika ni mchungu kwa sirikali, usishangae, wasambaa walishaainisha hayo.
 
sasa naamini yale maneno yanayosemwa sana mitaani, kuwa kuna watu wanaompa kipanya mawazo ya kuchorea picha ilikujiweka sawa kisiasa.
 
Kachemka Kipanaya au character wake? BTW Tanga itakuwa ya kwanza kujitoa maana iliungana na Nyika (pori) kuunda Tanganyika....nyika imetokana na neno la kijerumani nieker maana yake pori

Tanga ndo ilipaswa kuwa mji mkuu wa Tanganyika!
 
Mahesabu yako hivi:
-Zanzibar ni mkoa katika muungano
-Zanzibar ikijitoa kwa njia ya kura ya maoni,
-Ni sawa na mikoa mingine kuomba kujitoa kwa njia hiyo hiyo
-Kwa hiyo, hakuna kura ya maoni kwa Zanzibar
-Ili Mikoa mingine isiige mtindo huo mbaya

Baija unanichanganya.. Kama zenji ni mkoa mbona kuna rais, mawaziri, wakuu wa mikoa na wimbo wao wa Taifa? nieleweshe mkuu...
 
Back
Top Bottom