dickchiller
JF-Expert Member
- Apr 30, 2012
- 1,847
- 3,149
Kipa wa Mbao FC, Erick Ngwengwe amesimamishwa kuitumikia timu hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhujumu timu katika mechi yao dhidi ya Simba.
Mechi hiyo ilichezwa juzi Jumatatu kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo Simba ilishinda mabao 3-2.
Baada ya mechi hiyo kuliibuka taarifa za kwamba kipa huyo amehujumu timu kwa madai ya kwamba alipokea rushwa kutoka Simba. Mbao ilikuwa ikiongoza bao 2-0 hadi mapumziko ambapo Simba walirudisha mabao hayo na kufunga la ushindi kipindi cha pili.
Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi amethibitisha juu ya hilo na kwamba ikibainika kuwa alipokea rushwa basi ataondolewa kikosi moja kwa moja.