Kiongozi wa upinzani Mali, Soumaila Cisse afariki kutokana na Corona

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kiongozi wa upinzani nchini Mali Soumaila Cisse, aliyekuwa ametekwa nyara na makundi ya wapiganaji kwa muda wa miezi sita, amefariki dunia.

Kulingana na familia yake, Cisse amefariki akiwa nchini Ufaransa baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Alikuwa na umri wa miaka 71. Alikuwa amepelekwa Ufaransa kwa matibabu maalum baada ya kugundulika kaambukizwa virusi vya Corona.

Cisse alitekwa nyara mwezi Machi tarehe 25 na watu wasiojulikana, alipokuwa katika kampeni wakati wa uchaguzi wa wabunge, katika eneo la Timbukutu, kaskazini magharibi mwa Mali.

Aliachiliwa huru mwezi Oktoba, miezi sita baada ya kuzuiliwa na wapiganaji.

Aliachiliwa pamoja na raia wa Ufaransa Sophie Petronin na watu wengine wawili, raia wa Italia.

Wote waliachiliwa baada ya serikali ya Mali kukubali kuwaachilia huru wapiganaji 200, kufuatia ombi la makundi ya wapiganaji.

Cisse alishindwa katika uchaguzi wa rais nchini Mali, mara tatu.

Mwaka 2013 na 2018, alishindwa na Ibrahim Boubacar Keita, ambaye alipinduliwa na jeshi Agosti tarehe 18 mwaka huu.
 
Serikali ilikubali kunegotiate na magaidi ili kulinda maisha ya mpinzani? Mali wana political and social harmony ya kiasi hichi?

Huyo raia mwingine am sure hakufanya hizo negotiation ziwezekane as serikali ingeweza mtumia kama kigezo cha kugewa msaada na ufaransa kupambana na hayo magaidi.

Anyway ni move mbovu kidogo. Watateka mtu mwingine na kuanza kutoa maombi mengine zaidi.
 
Hakuna nchi haiwezi fanya hii negotiation. Hata kubwa la maadui Israel ilifanya hii kwa Hezbollah wakati inapiga marufuku kufanya mazungumzo na magaidi, hawa huwa wanaexchange hata maiti unakuta Israel inapokea maiti tano na kuachia wapiganaji 40. US kafanya sana hii na Taleban. Russia dhidi ya waasi wa Chechen aliwahi vamia kuokoa ili kukwepa matakwa yao matokeo yake wakafa watu wengi.
 
Israel walifanya operation entebbe kuokoa watu wao.

Naamini wao kuachia wapiganaji ili wagewe maiti ni wao ndiyo wameanzisha negotiation kudai maiti.
 
Israel walifanya operation entebbe kuokoa watu wao.

Naamini wao kuachia wapiganaji ili wagewe maiti ni wao ndiyo wameanzisha negotiation kudai maiti.
Operation ya Entebbe ni mojawapo kati ya matukio mengi ambapo raia wa Israel walitekwa. Sio kila mateka waliokolewa na operation, inategemea nchi gani walikuwa. Mfano Egypt iteke raia kisha Israel ilete ndege ya wanajeshi kwao. Sasa si itaongeza mateka. Hawa Uganda kwanza uwanja wenyewe ulijengwa na Waisrael na baadhi ya training kwa majeshi walitoa wao. Hao Hezbollah ilibidi itokee vita kabla ya exchange kufanyika.

Negotiations baina ya Waarabu na Israel zilifanyika nyingi na swaps zilitokea.
 
Back
Top Bottom