Kiongozi wa upinzani, Dkt. Kizza Besigye kutogombea Urais 2021

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Chama cha The Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda kimejipata katika njia panda baada ya muasisi wa chama hicho na mgombea mara nne wa urais , Kizza Besigye, kukataa ombi la kupeperusha tena bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa ujao wa 2021.

Dkt Besigye, ambaye alipambana na rais Museveni katika chaguzi nne za urais zilizopita tangu mwaka 2001, kila mara alimshutumu Rais huyo kuiba kura.

Alikwenda mara mbili katika Mahakama ya juu mwaka 2001 na 2006 na katika kesi zote hizo kwa kauli moja majaji walithibitisha kuwa kulikua na wizi wa kura lakini kwa mgawanyiko wa kura mwaka 5:2 na 4:3 mwaka 2006 , huku wengi wa majaji wakiamua kuwa wizi wa kura haukutosha kubatilisha matokeo ya mwisho ya kura.

Uamuzi wa Dkt. Besigye wa kutogombea urais mwaka 2021 umekiacha chama cha FDC kikimtafuta atakayekiwakilisha katika uchaguzi huo.

Tayari chama hicho kimeaihirisha mara mbili uteuzi wa wagombea wake wa uraiskwa matumaini kuwa Dkt. Besigye angebadili msimamo wake na kuchukua fomu za uteuzi.

2019 mbunge wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi na mwanaharakati wa kisiasa na mpinzani Dkt Kizza Besigye waliahidi kushirikiana kukiondosha madarakani chama tawala National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.

Chama tawala cha NRM kimekuwa madarakani tangu 1986.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha NTV, Bwana Besigye alikataa kujibu swali juu ya iwapo atagombea urais 2021 au la. Mara nyingi alisisitiza kuwa swali hilo ni kosa. Alisema hakuna uchaguzi utakaomg'oa madarakani Rais Museveni.

"Hatuhitaji uchaguzi ili tupate uhuru. Mkakati unaopaswa kutuandaa kupigana kwa ajili ya nchi yetu uchaguzi awepo au bila uchaguzi," alisema Dkt Besigye ambaye ni mpiganaji wa zamani na daktari binafsi wa Museveni wakati wa vita vyao vya msituni vya kati ya mwaka 1981 hadi 1986 vilivyoweka madarakani vuguvugu la National Resistance Movement (NRM).

Safari ya kutaka kuwania kiti cha urais nchini Uganda ya Dkt Kizza Besigye haikuwa rahisi. Mara kwa mara alikatwa kufungwa na hata kupigwa na maafisa wa usalama hususan alipojaribu kutafuta haki juu yake ukweli kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais

Mwaka 2016 Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) tena na maafisa wa polisi.

Watu walioshuhudia kukamatwa kwake walisema alikamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.

Alikamatwa baada ya kuwa kwenye kizuizi cha nyumbani wakati polisi walipomtuhumu kuwa alipanga kupanga kujitangazia matokeo.

Besigye alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Kira Road, Kampala baada ya kukamatwa.

Kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais, kabla ya kukamatwa kwake.

Bwana Besigye alikuwa mstari wa mbele kupinga muswada wa mwaka Januari mwaka 2019 wa kufuta kikomo cha umri wa miaka 75 ambao ulikuwa sheria Disemba 2017 ulihojiwa kwenye mahakama ya juu kabisa nchini Uganda.

Hata hivyo sheria hiyo ilipitishwa na Bunge na hivyo kumpatia fursa hasimu wake kugombea tena Urais na kumnyima fursa ya kupata kiti hicho cha ngazi ya juu zaidi nchini Uganda.

Katika mahojiano yake na BBC 2019 Bwana Besigye asema kuwa aliamua kujiunga na mwanasiasa mwingine wa upinzani na mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya utawala wa rais Museveni.

Polisi walisema alishikiliwa kwasababu ya kutotii amri za kutovuruga usafiri katika jiji la Kampala.

Bwana Besigye amekua akimuelezea Bwana Museveni kama ''dikteta''.
 
Back
Top Bottom