Kiongozi wa Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi yuko wapi?

Kiongozi wa Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi yuko wapi?

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,312
Hassan Hassan Taarisi ya Tahrir kuhusu Sera ya Mashariki ya Kati

_96513416_mediaitem96513414.jpg

Baghdadi alionekana hadharani mara ya mwisho 2014 mjini Mosul
Miaka mitatu iliyopita, video ilitolewa ya kiongozi wa kundi linalojiita Islamic State (IS), Abu Bakr al-Baghdadi, akiwataka wapiganaji wa kundi hilo wamtii katika hotuba aliyoitoa katika msikiti mkubwa wa al-Nuri mjini Mosul.

Mji huo wa Iraq ulikuwa umetekwa tena na wapiganaji wa kundi hilo na wakatangaza dola ya Kiislamu.

Wakati huo, IS, walikuwa wanadhibiti eneo la ukubwa sawa na Uingereza, lakini tangu wakati huo muungano wa majeshi ya nchi mbalimbali duniani umewakabili wapiganaji hao na kupunguza sana maeneo wanayoyadhibiti.

Bado haijulikani alipo Baghdadi, ambaye Marekani wametoa zawadi ya $25m kwa atakayetoa habari za kusaidia kupatikana kwake.

Wakati huu ambapo ni miaka mitatu tangu kutolewa kwa hotuba ya kwanza hadharani ya Baghdadi, na yake ya mwisho, IS hawadhibiti tena maeneo ya ardhi ambayo walidhibiti awali na kiongozi huyo wao amesalia kimya tangu alipowahutubia kwa kanda ya sauti Novemba mwaka jana, baada ya vita vya kuukomboa mji wa Mosul kutoka kwa IS kuanza.

Kumekuwa kukitolewa taarifa za kifo cha Baghdadi siku za karibuni, huku kimya chake kikizidi.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi alisema kuna uwezekano mkubwa sana kwamba aliuawa kwenye shambulio la kutoka angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Urusi mjini Raqqa tarehe 28 Mei.

Na afisa wa Iran alisema wiki iliyopita kwamba "bila shaka alifariki".

Hata hivyo, maafisa wa Marekani wametilia shaka madai hayo.

Kwenye video kutoka Raqqa wiki moja baada ya taarifa kutoka kwa Urusi, wapiganaji wa IS walizunmza kuhusu "sheikh wetu" bila kutaja jila la Baghdadi, na kuacha bado kukiwa na utata kuhusu hatima yake.

Si jambo la ajabu kwani Taliban na al-Qaeda pia walificha habari kuhusu kifo cha kiongozi wa Taliban Mullah Omar kwa miaka miwili.

Kwa wafuasi wake na maadui zake, ni jambo la kushangaza kwamba Baghdadi amesalia kimya.

'Mji mkuu wa tatu'

Jibu la kuhusu ni wapi Baghdadi yupo huenda likahusiana na madai yake kuhusu uhalali wake kama Khalifa au "kamanda wa waumini".

Kwa mujibu wa kanuni moja yeye utata wa kidini, mtu anaweza tu kujidai kuwa Khalifa iwapo ana "ardh tamkeen", au "ardhi ya kutawala".

Leo hii, ardh tamkeen inadidimia. IS kwa sasa ni kama karibu wameshindwa Mosul na pia wanashambuliwa vikali Raqqa, miji miwili ambayo wamekuwa wakiitumia kama miji mikuu yao Iraq na Syria.

Kama ishara ya kutambua utawala wao ulikuwa unakaribia kikomo Iraq, IS walilipua msikiti wa al-Nuri wiki mbili zilizopita kabla ya wanajeshi kuteka eneo hilo.

Baghdadi huenda akawa mafichoni katika eneo ambalo limeelezwa kama "mji mkuu wa tatu wa IS", maeneo ambayo yanadhibitiwa na kundi hilo katika mpaka wa Syria na Iraq.

IS huita eneo hilo Wilayat al-Furat, au "Mkoa wa Euphrates", eneo ambalo linajumuisha mji wa Iraq wa al-Qaim na mji wa Syria wa Albu Kamal.

Mwaka 2014, IS walianza kwa kudhibiti Wilayat al-Furat na maeneo ya karibu.

Kwa mujibu wa kundi hilo, kupitia video walizotoa juzi kutoka mkoa wa Anbar nchini Iraq, wapiganaji hao walitumia eneo hilo kutekeleza mashambulio ya kasi sana Iraq na Syria.

Chanzo: BBC Swahili
 

Attachments

  • upload_2017-7-4_16-7-58.gif
    upload_2017-7-4_16-7-58.gif
    51 bytes · Views: 39
Duuuh,,,,,,,huyu mtu kama wamemuua basi hongera zao
 
Anaitwa Professor Alhadji Dr. Caliph Abuu Bhakar Al Baghdadi msaidizi wa mtume.

Anasema yeye ni next to Mtume Mohamed, kwanza kwenye organization structure ya Allah, yeye ni wa tatu katika ile seniority/chain of command. Wa kwanza allah mwenyewe, wa pili Mtume mohamed na wa tatu yeye Baghdadi.

Na alipotangaza dola ya kiislam mwaka 2013 aliwataka waislam wote ulimwenguni kumuheshim na kumlinda kama wanavyomheshim mtume, kwamba yeye ndie muwakilishi wake Duniani.

Hivyo atakua mahala salama huku kukiwa na ulinzi aa kutosha kwa waislam walioamua kwa hali na mali kumlinda khalif wao asizurike.
 
mpuuzi mmoja hivi anaeingiza waislam kwenye matatizo!! All in all hizo zote ni Ajenda
 
Russia na Iran waongo tu
Kama hajaonekana toka 2014 iweje wao leo waseme wamemuua
 
Back
Top Bottom