Kiongozi wa IS auwawa Syria

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
150513202454_al-afari__640x360_na_nocredit.jpg

Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu, vyombo vya habari vya Marekani vimesema.

Maafisa wa ulinzi wameliambia shirika la habari la NBC kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa Iraq anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi mwezi huu.
Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.

Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.
Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu mwaka 2014.

Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul kulingana na Marekani.
Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.

Source: BBC Swahili
 
afadhali wapungue hao chinjachinja
 
Waongo hawa, wanaona Russia anawamaliza wanaanza kuzuga kuua viongozi wakati wanawaficha
 
We umeshambiwa kauawa..ka yupo hai basi Russia aseme yupo hai bado..Au wewe unayebisha ulete ushahidi kwamba yupo hai..
Otherwise shut tha f**ck up..
 
mbona unantukana ase, hamna noma.
 
Back
Top Bottom