Kiongozi wa FDLR afungwa miaka 13 Ujerumani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,569
Reaction score
53,583
150928130006_ignace_640x360_bbc_nocredit.jpg

Mahakama moja ya Ujerumani imewahukumu viongozi wawili wa waasi nchini Rwanda kwa kupanga njama za kushambulia raia katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ignace Murwanashyaka na Straton Musoni wanatuhumiwa kwa kuwaagiza wapiganaji kufanya mauaji ya halaiki pamoja na ubakaji kati ya mwaka 2008 na 2009.

Kesi yao ilifanyika chini ya sheria ambayo inaruhusu kuwashtaki wageni kwa uhalifu ulioyafanyika nje ya taifa la Ujerumani.

Hatua hiyo ilionekana kama ushindi dhidi ya waasi waliotekeleza uhalifu nchini Rwanda.
Murwanashyaka,ambaye ni kiongozi wa kikosi cha FDLR alipewa hukumu ya miaka 13 huku Musoni ambaye ni naibu wake akihukumiwa mika 8 jela.Hatahivyo Musoni ameachiliwa huru kutokana na miaka aliyokuwa akizuiliwa.

Uwepo wa FDLR mashariki mwa Congo ni moja ya maswala yanayosababisha mizozo ya miaka nenda miaka rudi nchini humo na kusababisha vifo vya watu milioni tano katika eneo hilo.

Wawili hao waliokamatwa ,mwaka 2009 wamekuwa wakiishi nchini Ujerumani tangu mapema miaka 1990 na kutoka huko walipanga mashambulizi dhidi ya raia mashariki mwa Congo.

Walishtumiwa kwamba waliagiza mauaji ya watu kwa kukataa kushirikiana na FDLR.

Wakati wa kuanza wa kesi hiyo miaka minne iliopita,kiongozi wa mashtaka wa Ujerumani Christina Ritscher alisema kuwa wawili hao walikuwa wanajua kila kilichokuwa kikiendelea.

Chanzo: BBC Swahili
 
Very good...hawa ndio Jmali and his irk sleep and eat JF defending their evils,wako wengi bado wanakimbia kimbia lakini one at a time watapata justice yao,Jmali upo?
 
I fully support justice regardless ya nani anahusika. Most people support FDLR's position on Rwanda na sio just kila kitu wanachofanya hata kama ni uhalifu. We supported talks and disamarment on one hand, lakini walipokataa tuliruhusu wapigwe na Monsuco, see? Muhimu katika hili ni kuwa walipelekwa mahakamani kwa makosa yao, hawakuhukumiwa extradujiciary. Pili, mashtaka yao hayahusiani na harakati zao kuhusu Rwanda, don't get it twisted, hawajahukumiwa for "genocide", "terrorism" wala tuhuma zingine za kutungwa na kagame, wamehukumiwa kwa other crimes committed in DRC. So i guess this is one of few times where me and you agree on something. Sasa kwa vile hii inahusu crimes in DRC, why not join me kufuatilia yet another DRC-related case, ICC vs Bosco Ntaganda of M23? Ili na yenyewe wapenda amani kama mimi na wewe tushangilie verdict? what do you say? :mvutaji:
 
Actually mimi sijashangilia hukumu hii....i wanted them to be brought to Rwanda and
face genocide charges that are awaiting them. Labda baada ya kutumikia hiki kifungo wataletwa huku tuwaongezee miaka mingine ndani.
 
Do you also support M23 na Laurent Nkunda warudishwe DRC to face justice too?
 
is sultan makenge facing somekind of trial in rwanda?
 
Back
Top Bottom