Kiongozi wa Chaso (CHADEMA) UDOM aachiwa huru

Kiongozi wa Chaso (CHADEMA) UDOM aachiwa huru

tajirijasiri

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,863
Reaction score
3,854
Hivi unaanzaje kumshikilia mtu kwa tuhuma za kuwashawishi watu kujiunga na chama chake cha siasa?

Kumbuka hajalazimisha, ila ameshawishi. Au kwa sababu ni chama cha upinzani (Chadema) na sio chama tawala (CCM). Kumbuka ipo siku CCM kitakuwa chama cha upinzani pia.

Haijalishi ni lini, lakini muda utafika. Hakuna utawala uliodumu milele.

Tenda haki.

===
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chaso) wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) nchini Tanzania, Henry Mang’era ameachiwa huru leo Jumatatu Desemba 2, 2019 baada ya kushikiliwa kwa siku tatu na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na siasa ndani ya chuo hicho.

Baada ya kuachiwa, Mang’era aliyekamatwa na polisi tangu Ijumaa iliyopita ya Novemba 29, 2019 na kuachiwa leo Jumatatu, kilifanyika kikao kati yake na uongozi wa Udom.

Polisi walipokamata walimnyima dhamana mwanafunzi huyo kwa madai ya kuhatarisha usalama chuo hapo kwa kuwashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunga na Chadema.

Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Uhusiano wa Umma na Masoko wa Udom, Prudence Rwehabura amekiri kushikiliwa na polisi lakini si kwa wiki mbili kama ilivyoandikwa kwenye mitandao ya jamii.

Amesema mwanafunzi huyo alikamatwa Ijumaa na kuachiwa leo na baadaye kuwa na mazungumzo na uongozi wa chuo.

Amesema baada ya mwanafunzi huyo kuonyeshwa sheria ndogo ndogo inayokataza wanafunzi kujishughulisha na siasa ndani ya chuo, alikiri na kumsamehewa.

"Amekiri na kusema kuwa hatarudia tena kosa hilo, uongozi wa chuo umemsamehe.

Na amejaza fomu ya kuonyesha hatarudia tena, kwa hiyo hilo limekwisha na anaendelea na masomo yake kama kawaida, amesema.

Source: Mwananchi
 
Ukiwa na madaraka au pesa utadanganywa sana kwamba unapendwa sana na kuheshimiwa na kuitwa mheshimiwa mtukufu. My dear. Hebu siku pesa ziishe na usiwe na madaraka utaonekana kama haja kubwa ya mlevi wa mnazi. Nina ushahidi kwakua nimeyaona kwangu binafsi.
Uganda kulikua na Conqueror.
 
Umenena mkuu...
Ukiwa na madaraka au pesa utadanganywa sana kwamba unapendwa sana na kuheshimiwa na kuitwa mheshimiwa mtukufu. My dear. Hebu siku pesa ziishe na usiwe na madaraka utaonekana kama haja kubwa ya mlevi wa mnazi. Nina ushahidi kwakua nimeyaona kwangu binafsi.
Uganda kulikua na Conqueror.
 
Mbona CCM inafanya hivyo hivyo na hakuna anayekamatwa?
Unajua ukiwa kwenye usukani hutaki abiria yoyote akuelekeze kuendesha. Hata baba yako aliyenunua gari wakati hujajua kuvaa chupi unamuona hajui udereva kama wewe.
Nasemaga tu " Time is a brutal tireless teacher" Rejea ndoto ya NABUKADREZAR.
 
Back
Top Bottom