Kiongozi ni bora kuliko Meneja

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
996
742
TOFAUTI YA MANAGER NA LEADER. KIONGOZI NI NANI?


Kama unataka kujua nini tofauti ya leader (kiongozi) na manager (msimamizi) basi leo kuna machache ya kujifunza hapa. JIPIME, JIKOSOE na CHUKUA HATUA.

KIONGOZI AU LEADER NI NANI?

Kiongozi ni mtu anayeonyesha njia, mara nyingi njia hiyo huwa ni yeye ndiye aliyeigundua, au kuitengeneza au kuitambulisha kwa watu, kikundi cha watu au jamii inayomzunguka. Ni vizuri kujua kwa kina tofauti iliyopo kati ya kiongozi na msimamizi ili ya kwamba ujue wewe ni nani? Kwa kimombo kiongozi ni leader na msimamizi ni manager.

KIONGOZI kwa kawaida hufanya vitu sahihi au vitu vinavyohitajika na watu au jamii kwa muda huo. Doing right things -Drucker.
Kiongozi huunda wazo/ono (vission), na kulifanya kuwa bidhaa inayohitajika na watu na kisha kuunda timu ya watu na mali, pamoja na mitambo (organise resources) itakayotumika kuunda bidhaa hiyo . Kiongozi huona mbali kuliko mtu yeyote - see beyond normal eyes.
Kiongozi huwa na MAONO, DIRA na MWONGOZO wa kufika huko anataka kufika. Kiongozi huwa amehamasika daima hata pale anapopitia wakati mgumu.

TAFAKARI. Una Maono? Dira? Mwongozo? Je malengo yako ni yapi? Umeunda nini? Unaongoza watu wangapi na je wamefanikiwa? Kama jibu ni NO, sasa anza upya Jipange la sivyo Utapangwa

Sasa kiini (key) cha tofauti ya kiongozi na msimamizi au meneja kinatokana na nini wanafanya na wanafanyaje. Angalia leader anafanya vitu sahihi, anaweka malengo na kutafuta mbinu za kutimiza malengo ikiwa ni pamoja na kuajiri watu mfano meneja. Leader ana fanya vitu sahihi na kuwaachia mameneja na wasimamizi kufanya vitu kiusahihi (doing things right). Leader anamwekea msimamazi vigezo au viwango vya utendaji au matokeo (KPI - Key Performance Index). Leader atakuwa anaangalia je kampuni yangu, biashara mradi/project inaelekea ninakotaka iende? Au inachepukachepuka. Leader atazama ndani zaidina kuona ni kwa namna gani mazingira ya ndani na nje ya biashara au mradi yanamletea faida au hasara - SWOT analysis. Na kisha kumwelekeza meneja nini cha kufanya. Leader anakuwa macho muda wote.

Siku zote leader anakuwa na majibu (proactive) ya hali mbalimbali zinazoweza jitokeza sasa au baadae kumpinga au kumwongeza kibiashara.
Leader ni mmiliki wa mradi, biashara au shuhuli, akifa mradi unayumba au inabidi uumbwe upwa.
Leader ni mshawishi ambaye anaouwezo wa kuelezea fikra nzito na ngumu na jamii ikamwelewa, ikamuunga mkono na pia kununua au kujiunga na mradi wake kwa kutegemea kujifunza kutoka kwa leader au kupata ujira au sifaa tu. Si unakumbuka wakati wa kampeni kuelekea December 25. Kulikuwa na Team Edo, Team Pombe nakadhalika.

Tofauti ya mwisho kwa Leo of course zipo nyingi ni kwamba leaders ni wasanii (artist) wazuri wanajua kubadilisha mazingira mbalimbali ili yaendane na maono yao, hii ni pamoja na kutoa story mbalimbali zenye kuwavuta watu wawafuate - 'follow me' na kuwasililiza 'like my page' Leader yeyote hata kama ni mkimya kiasi gani wakati anaelezea jambo gumu lazima ataweka mfano au story, pia atachekesha, kukaripia, kusifia na kuonya - JK Nyerere ni mfano mzuri.
Jiulize 'are you inspiring au unapifapiga domo tu kama Mwalimu wa Karate?


MBINU ZA KUWA KIONGOZI BORA KWA KIFUPI.
ILI UWE KIONGOZO BORA


1. HAKIKISHA UNAWAPA WATU MATUMAINI YA BAADAYE

Create an inspiring vision, kuwa miongoni mwa watu wanaotegemewa kutoa majibu ya matatizo na maswali yanayoikabili jamii, waelezee watu kiurahisi product yako na jinsi ilivo na msaada kwao.


2. WAHAMASISHE WATU KUJIUNGA NAWE NA KUWA NA MAONO KAMA YAKO


Elimu, Elimu, Elimu bila kuchoka wape elimu. Waeleze faida, usitie chumvi, waelezee mafanikio yako hata kama ni kidogo, wape visa vya watu duniani waliokuwa na dhiki lakini kwa kutimia mbinu unayowapa wamefanikiwa.


3. ELIMU NA UJUZI.


Hakikisha unayabeba maono na kuangalia kila siku kama mwelekeo wa matendo yako na timu yako ni sahihi, au kuna michepuko. Kama umeajiri watu wape vigezo au KPIs. Hudhuria semina na hamasisha watu wako kuhudhuria semina bila kukosa. Soma vitabu na angalia movie za masomo sio Egol na Mara Crala. Hudhuria semina, jifunze, chunguza waliofanikiwa wamefanya nini..


4. JENGA TEAM - TEAM BUILDING.


Katika karne hii teams ndio kila kitu, ukiwa na timu mbovu ya Mpira kama iliyokuwa Chelsea kazi yako itakuwa kutoa mpira golini. Kiongozi lazima uwe na uwezo wa kujenga timu yako imara inayoweza kufunga magoli (cash inflow) na kuzuia kufungwa (cash outflow). Jenga team kubwa ipe mbinu (success tools) na wape motisha, wewe na timu yako mtafanikiwa.





Makala hii ipo Price Watch Afrique katika ukurasa wa Uongozi

AU BOFYA HAPA
Price Watch Afrique: TOFAUTI YA MANAGER NA LEADER. KIONGOZI NI NANI?
 
Back
Top Bottom