Kiongozi gani wa dini anayemshauri...

Kiongozi gani wa dini anayemshauri...

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
ANASHANGAA MHESHIMIWA LISSU KUSHAURIWA NA ASKOFU KWA KUWA HAMJUI ASKOFU ANAYEMSHAURI RAIS MAGUFULI!

Ukiongea na Askofu Mwamakula uwe makini sana kwa sababu anatunza kumbukumbu vizuri. Hebu fuatilia mazungumzo yake na mmoja wa viongozi wa dini siku kadhaa zilizopita.

Kiongozi wa Dini: Nimesikia kuwa wewe ni Askofu Mshauri wa Tundu Lissu! Ni kweli? Leo nataka nikusikie kwa kinywa chako.

Askofu Mwamakula: Sahihi

Kiongozi wa Dini: Kwa nini?

Askofu Mwamakula: Kwani ni dhambi kwa Askofu kuwa Mshauri wa Mgombea Urais?

Kiongozi wa Dini: Sio dhambi! Lakini huoni kama hiyo itakuwa ni hatari sana kwako na kwa Kanisa lenu?

Askofu Mwamakula: Ni hatari kwa mgombea Urais kushauriwa na Askofu? Ulitaka ashauriwe na wachawi au waganga wa kienyeji?

Kiongozi wa Dini: Hapana! Lakini kuwashauri wapinzani ni hatari sana katika mazingira ya sasa! Utaonekana kama unapingana na Serikali.

Askofu Mwamakula: Kwani wapinzani sio Watanzania?

Kiongozi wa Dini: Ni Watanzania
Hivi wewe huogopi lakini?

Askofu Mwamakula: Siogopi! Kwani katika Biblia, Wafalme walikuwa hawashauri na manabii?

Kiongozi wa Dini: Walikuwa wanashauriwa kabisa.

Askofu Mwamakula: Hivi unamjua Askofu Mshauri wa Rais Magufuli?

Kiongozi wa Dini: Hivi kweli yupo? Simjui!

Askofu Mwamakula: Ukiombwa wewe uwe mmoja wa Viongozi wa Dini Washauri wa Rais Magufuli utakubali?

Kiongozi wa Dini: Ha ha ha! Kwa nini nikatae kama kuna uhitaji?

Askofu Mwamakula: Haitakuwa hatari kwako?

Kiongozi wa Dini: Ha ha ha! Kwa kuwa nitakuwa nashauri serikali haitakuwa hatari.

Askofu Mwamakula: Mheshimiwa Lissu akiingia madarakani utakuwa tayari kuwa mshauri wake?

Kiongozi wa Dini: Hapo hakuna shida.
 
Kwani wapi palipoandikwa ameingia madarakani? Kama si wizi wa polisiccm na tume fake ya uchaguzi matokeo halali ya uchaguzi unayajua. Acha kujitoa ufahamu!
Bwana Lissu hakuingia madarakani! Na hapo ndipo palipo kuwa na shida!
 
Saa nyingine huwa nahisi hawa maaskofu Mwamakula na Bagonza wanalishwa maneno. Anayeletaga habari zao ni yule yule tena usiku usiku na akipotea jukwaani miezi 6 na hizi ngonjera zinaenda likizo mpaka arudi. Trying to connect dots...
 
Back
Top Bottom