Kiongozi anapokuwa mwananchi wa kawaida! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi anapokuwa mwananchi wa kawaida!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jan 21, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tumekuwa na awamu nne sasa za uongozi:Mchonga,Mwinyi,Mkapa na Kikwete.Mungu aibariki sana awamu ya Mchonga.Ilikuwa awamu yenye authority,Mchonga akisema kitu kisifanyike kweli hakifanyiki.Huo ndio aina ya uongozi tulioupenda na ambao tunautaka.Uongozi wa aina hii umekwenda na Mchonga,leo tunauota tu kwenye ndoto.Sijui kama tutafika.

  Nchi yetu leo ina matatizo ya kutisha.Kinacho shangaza hata hivyo ni kwamba viongozi wetu wanaimba wimbo ule ule wanaoimba wananchi,wangefanya vile,wangefanya hivi, wangefanya vile,kana kwamba wao sio viongozi.Ajabu sana.Waziri wetu Mkuu majuzi,alikutana na makatibu wake wakuu.Wimbo ukawa ndio ule ule,mngefanya vile na hivi na vile,mambo yangekuwa mazuri,Tanzania tusingekuwa hapa tulipo.Nilidhani jamaa hajui matatizo ya Tanzania,duu,kumbe anayajua vizuri sana.Inashangaza sana.Mimi nilidhani kujua chanzo cha tatizo ndio mwanzo wa kulitatua,kumbe hiyo sio formula ya viongozi wa Tanzania.Katika hali iliyonishangaza zaidi,kule Karagwe ameopoa albino mmoja,ili akamlee,eti mazingira atakayokulia Karagwe ni magumu!Hivi albino wengine waliobaki mitaani atawalea nani?Mbona nao maisha ni magumu, na yako hatarini kama huyo wa Karagwe?Nadhani tunachohitaji ni mazingira ambayo albino wote na wanachi wote kwa ujumla wataishi kwa amani na matumaini,sio kuopoa mmoja mmoja halafu basi.Wimbo ulioimbwa kule Karagwe nako ni ule ule,mngevalia njuga swala la albino kama la majambazi,tatizo hili lingekwisha kabisa.Sasa Waziri Mkuu,jamaa hawajavalia njuga swala hilo kabisa, na kwa kweli hawana mpango wa kufanya hivyo kabisa,wewe kama Waziri Mkuu unasemaje?Mnge,Mnge,Mnge,kinachoendelea hakuna, albino wanaaangamia.Hivi ni lini viongozi wetu watatekeleza wajibu wao halali kama viongozi na ambao wamepewa na katiba?Hivi ni lini watafunga mapaka shume haya kengele yakome kuwatesa wananchi wetu?Hivi ni lini hasa watakuwa na authority?
   
  Last edited: Jan 21, 2009
Loading...