Jamaa alichungulia kwa kinyozi akauliza, "Nataka kunyoa nirudi baada ya muda gani?" Kinyozi akajibu,"Niko bizi rudi baada ya masaa mawili". Baada ya wiki jamaa akarudi tena, akauliza swali lilelile kinyozi akajibu,. "Rudi baada ya nusu saa".Wiki ya tatu akarudi akauliza tena swali lake , kinyozi akamjibu, "Rudi baada ya saa moja". Safari hii kinyozi akamwita mtoto mmoja akamwambia, "Hebu mfuate yule jamaa ujue anaenda wapi". Baada ya muda mtoto akarudi akamwambia kinyozi, 'Yule jamaa kaenda nyumbani kwako'
sasa jamaa mbona akiambiwa rudi baada ya muda fulani harudi katika huo muda? ama kwa kuwa anaenda nyumbani kwa kinyozi kunyolewa na wife wa kinyozi.
jamaa kinyozi na mkewe pia anahesabu vichwa.
Mkuu, Mbimbinho ukiona hivyo ndo kuchanganyikiwa huko. Usfanye mchezo na mke aisee. Nafuu tu nimwambie mi ni kinyozi express, vinginevyo niko hatarini!