Kinyesi kutoa harufu kali

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,558
21,035
Habari za leo wapenzi wa JF Doctor,

Kuna tatizo analo mfanyakazi wangu wa ndani la kujisaidia kinyesi chenye harufu kali sana kiasi kwamba kama akijisahidia harufu inatawala nyumba nzima mpk kero. Tumejaribu kumshauri anywe maji kwa wingi na kula vyakula laini na mapapai lakini bado haisaidii. Tumeishi nae kwa miaka mitatu sasa akiwa na hilo tatizo kiasi kwamba nafikiria kujenga choo cha nje kwa ajili yake maana amekuwa kama ndugu sasa.

Swali langu kwenu ni je kuna tiba yeyote juu ya tatizo hili? Naomba ushauri ndg zangu, serious
 
Miaka MITATU bado mnajaribu kubadilisha chakula? Mpeleke hospitali akapimwe. Kuna magonjwa ya tumbo na utumbo yanayosababisha kinyesi kunuka.
 
Miaka MITATU bado mnajaribu kubadilisha chakula? Mpeleke hospitali akapimwe. Kuna magonjwa ya tumbo na utumbo yanayosababisha kinyesi kunuka.
naliwahi kumpeleka hospitali ndio wakasema ajaribu kula vyakula laini na kutumia mapapai kila mlo, lakini hali bado ni tete kwa madaktari je mmewahi kukutana na kesi kama hiyo?
 
naliwahi kumpeleka hospitali ndio wakasema ajaribu kula vyakula laini na kutumia mapapai kila mlo, lakini hali bado ni tete kwa madaktari je mmewahi kukutana na kesi kama hiyo?

Ana umri gani? Ukiacha mapapai, anapendelea kula vyakula gani? maana kuna vyakula kama mayai, parachichi na baadhi ya vileo; ukivitumia lazima utatoa kinyesi chenye harufu kali.
 
Ana umri gani? Ukiacha mapapai, anapendelea kula vyakula gani? maana kuna vyakula kama mayai, parachichi na baadhi ya vileo; ukivitumia lazima utatoa kinyesi chenye harufu kali.

Kula chakula chenye mafuta mengi kunasababisha kinyesi chenye harufu kali. Hata hivyo, si kila siku tunakula vyakula vyenye mafuta mengi, hivyo wengi wetu tunapata hali hii mara moja moja. Mfano ukila chakula kwenye sherehe. Lakini kama imeendelea kila siku kwa miaka 3 hiyo si kawaida. Maelezo yake ni mengi, ingia google utaona. Ila cha muhimu mpeleke check up.
 
Jenga choo cha nje faasta.
Pia
1. Rudi hospital kwa dr mwingine bana
2. Suala la maji na vyakula lizingatiwe, awe anaamkia pawpaw moja, maji vuguvugu lita 2 then ndo breakfast. 3 weeks kwishney. Nidhamu ya hili muhimu
 
Wakati mwingine yafuatayo huchangia:1=kutokula mlo kamili, 2= kula kwa wingi vyakula vya barabarani, 3=kula vyakula vya protein kwa wingi kama maharagwe,maziwa,mayaink, 4= kula vyakula ambavyo myeyusho wake huchukua muda mrefu, 5=kutotulia baada ya kula kwa muda, mfano nusu saa au saa moja, 6= kula ukiwa safarini, 7=magonjwa ya tumbo , 8= kula vyakula venye vitamini kwa wingi hasa vikiwa havijapikwa nk, 10=kuzaliwa mtu na enzaimu na kemikali nyingine ambazo zinakuwa sababishi vikichanganyika na vyakula aina fulani mfano papai,parachichi,cabichi ,nk
 
Nilitaka niseme labda kuvimbiwa. But hili lisingekuwa tatizo la muda wote huo wa miaka mi3. Nenda hospital tofauti na ile ya mara ya kwanza.
 
Sijaelewa kwani kinyesi huwa kinanukiaga? Hiyo harufu kali ni kwa kipimo cha maabara? isije ikawa munampa ukoko na miba ya samaki na mikachumbali iliyo chacha. Tena mukionesha kuchoshwa na yeye kwa hilo mbele yake anaweza akachukua aftershave na manukato yenu anywe kwa siri, chukueni tahadhari. Si umsikia housegirl alipolaumiwa kuto tunza vizuri vijiti vya kuchokolea meno. ikawa kila akimaliza kutumia vijiti anarudishia katika mkebe wake ili asilaumiwe
 
niliwahi kusikia tatizo kama hilo...mpeleke hospitali kubwa atakuwa na tatizo la tumbo. Jaribu kumuuliza anaweza kukwambia tumbo huwa linajaa gesi muda wote. Achana na habari ya mlo kwani si kisababishi.
 
Hapa tatizo si chakula bwana, inaonekana anatatizo huyo binti hasa tumboni ama njia ya haja kubwa. inabidi akafanyiwe uchunguzi wa kina. Mpeleke hospitali za rufaa kama muhimbili na hasa muhimbili achana na hospitali uchwara
 
Sijaelewa kwani kinyesi huwa kinanukiaga? Hiyo harufu kali ni kwa kipimo cha maabara? isije ikawa munampa ukoko na miba ya samaki na mikachumbali iliyo chacha. Tena mukionesha kuchoshwa na yeye kwa hilo mbele yake anaweza akachukua aftershave na manukato yenu anywe kwa siri, chukueni tahadhari. Si umsikia housegirl alipolaumiwa kuto tunza vizuri vijiti vya kuchokolea meno. ikawa kila akimaliza kutumia vijiti anarudishia katika mkebe wake ili asilaumiwe

hapana nduguyangu house girl wangu anakula chakula kama tunachokula sisi na uwa tunakula familia nzima pamoja nae mezani labda useme asubuhi wakati sisi hatupo awe anakula viporo ingawa sidhani kama ndio inaweza kuleta tatizo kihivyo

Nitajaribu kumpeleka kwa daktari mwingine, kuhusu kunuka kinyesi najua vyote vina harufu ila hii imezidi yaani kama akijisahidia wakati mnakula harufu inakuwa kali mnaweza kuacha na yeye kwa kuwa amejistukia uwa anajisahidia usiku lakini hiyo harusu hata ukiwa usingizini utaisikia tu
 
Mmh giardia wamemkomalia huyo,cha muhim mpeleke refferal hospital co dispensary
 
Kuna chemikali inaitwa Bilirubin inapatkana kwenye nyongo, kazi yake ni kupunguza harufu ya kinyesi huenda ana tatizo la kutokuwa nayo ya kutosha .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom