Kinondoni yanyimwa mabilioni ya miradi

Kinondoni yanyimwa mabilioni ya miradi

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
SERIKALI imezuia Sh. bilioni 38 zilizokuwa zielekezwe kwenye utekelezaji wa miradi mitatu ya kimkakati ya kuijengea uwezo kimapato Manispaa ya Kinondoni, baada ya kubainika kuwa utekelezaji wa mradi wa soko la kisasa la Magomeni uliopatiwa zaidi ya Sh. bilioni 8.5, unasuasua.

Uamuzi huo ulitolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani Dar es Salaam. Katika ziara hiyo, alikagua miradi kadhaa ya kimkakati iliyopewa ruzuku na serikali na kubainika kuwa haitekelezwi kwa mujibu wa mikataba.

Miradi mitatu iliyoguswa na uamuzi huo wa serikali ni wa uendelezaji wa Ufukwe wa Oysterbay wenye thamani ya Sh. bilioni 14.1, Soko la Kisasa la Tandale (Sh. bilioni 9.7) na soko la Kisasa la Kibada (Sh. bilioni 14), yote ikiwa katika Manispaa hiyo ya Kinondoni.

"Hatutaleta fedha hizi ambazo ni utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya awamu ya pili ambayo Manispaa ya Kinondoni ilipewa ruzuku na mikataba yake kutiwa saini Februari 5, 2019 mpaka hapo tutakapojiridhisha na utekelezaji wa mradi huo wa soko la kisasa la Magomeni kwa sababu watendaji wanaosimamia mradi huo ni wale wale ambao wangesimamia miradi hiyo mipya mitatu," alisema.

wanaisimamia kwa karibu miradi yote ya kimkakati inayotekelezwa katika maeneo yao ili kutimiza dhamira ya serikali kuziwezesha mamlaka za serikali za mitaa kujitegemea ili kutoa huduma bora kwa wananchi. Pia Dk. Kijaji alionya kuwa miradi yote ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa nchini isiingizwe siasa ndani yake kwa kuwa itaharibu maana yake ya kuwa miradi ambayo serikali imeridhia kuipa fedha ili ianzishwe kwa ajili ya kuchochea maisha na uchumi wa wananchi.

Akiwa ziarani mkoani Dar es Salaam, Dk. Ashatu Kijaji, alikagua utekelezaji wa miradi ya kimkakati ambayo ni sehemu ya miradi 22 ya awamu ya kwanza ambayo serikali ilitoa ruzuku ya zaidi ya Sh. bilioni 147 Mei, mwaka jana 2018, ukiwamo mradi wa masoko ya kisasa ya Kisutu, Mburahati na Magomeni, ujenzi wa Kituo cha Mabasi Mbezi Louis na machinjio ya kisasa Vingunguti.

Akiwa katika soko la Kisutu, Dk. Kijaji alielezea kutoridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa soko hilo na kuutaka uongozi wa wilaya na Manispaa ya Ilala kuongeza kasi ya ujenzi wa soko hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa wilaya hiyo.

Katika soko la Magomeni, alitangaza kuzuia Sh. bilioni 5.5 ambazo zilipaswa kutumika kutekeleza mradi wa kimkakati wa soko hilo lililoko wilaya ya Kinondoni, kutokana na kucheleweshwa kwa utekelezaji wa mradi huo licha ya kupewa Sh. bilioni tatu za kianzio miezi kadhaa iliyopita. Aidha, akiwa Vingunguti, alitangaza kuinyang'anya Manispaa ya Ilala, Sh. bilioni tatu ilizoipatia kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kimkakati wa machinjio ya kisasa wa eneo hilo baada ya Manispaa hiyo kushindwa kuanza kutekeleza mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 8.5.
 
Ni logical alichokisema naibu waziri; ila pia ni kuwa hata hiyo hela yenyewe haipo. Serikali ya jiwe imefulia.
 
Kama vile hakuna pesa na hii ndio njia ya kusogeza mbele muda wa utekelezaji mradi wakisubiria pesa.
 
Back
Top Bottom