Kinondoni, Dar: Marufuku kupiga muziki kwenye baa bila 'Sound-proof'

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
22d667e0-d49c-44ea-898c-92cd798b2cb4.jpg
 
Kwenye hili la muziki wa kelele naunga mkono hoja mia kwa mia.. Kuna bar ya mwanajeshi hapa jirani na kwangu ni baraa unaporomoshwa mziki kama tupo night club,hata ukienda kutoa taarifa bure wanakuja watu wa Halmashauri na Polisi wanachomewa mbuzi na kupatiwa hela ya vocha na story inaishia hapo
 
Kwani hizo mamlaka zinataka nini??? Kama ni ofic za serikali zinafungwa sa9.30 mtu akienda bar sa10 tatizo liko wapi? Siku za wkend unaagizaje bar kufunguliwa jioni namna hiyo? Waache maamuzi ya kukurupuka ambayo mwisho wake yanaleta ugumu ktk utekelezaji. Asiyewajibika kwa ulevi ataonekana huko ofisini kwake na atumbuliwe huko...tunataka nchi ya viwanda sasa hata hivi vilivyopo tunataka kuviua kwa maamuzi yasiyo na busara. Maamuzi ya ilimradi mtu aonekane na yeye amesema kitu ili MKULU amkubali katika ufalme wake. Ndooroooobooooo
 
Wanataka kuwapa sababu TBL kukwepa kodi tu,kwani mtu kama ana shughuli au kazi yake muhimu hawezi kuacha eti aende kunywa pombe,siungi mkono utaratibu huo

Ukikiuka wanakupiga tanganyika jack mkuu
 
Wanataka kuwapa sababu TBL kukwepa kodi tu,kwani mtu kama ana shughuli au kazi yake muhimu hawezi kuacha eti aende kunywa pombe,siungi mkono utaratibu huo

Kwa hiyo tukusadiaje sasa kama hauungi mkono??
 
Kwani hizo mamlaka zinataka nini??? Kama ni ofic za serikali zinafungwa sa9.30 mtu akienda bar sa10 tatizo liko wapi? Siku za wkend unaagizaje bar kufunguliwa jioni namna hiyo? Waache maamuzi ya kukurupuka ambayo mwisho wake yanaleta ugumu ktk utekelezaji. Asiyewajibika kwa ulevi ataonekana huko ofisini kwake na atumbuliwe huko...tunataka nchi ya viwanda sasa hata hivi vilivyopo tunataka kuviua kwa maamuzi yasiyo na busara. Maamuzi ya ilimradi mtu aonekane na yeye amesema kitu ili MKULU amkubali katika ufalme wake. Ndooroooobooooo

Kwani ukitoka kazini ukapitia bia zako na kwenda kunywea nyumbani kuna ubaya gani? Kwanza itakusaidia hata kuboresha mahusiano ya kifamilia!
 
Kwenye hili la muziki wa kelele naunga mkono hoja mia kwa mia.. Kuna bar ya mwanajeshi hapa jirani na kwangu ni baraa unaporomoshwa mziki kama tupo night club,hata ukienda kutoa taarifa bure wanakuja watu wa Halmashauri na Polisi wanachomewa mbuzi na kupatiwa hela ya vocha na story inaishia hapo
Hili la muziki wa kelele ni janga la kitaifa. Pale Matosa kuna jamaa, mziki mnene utafikiri Club halafu mbaya zaidi wateja wenyewe wakuunga unga lakini ndio sauti kubwaaa utafikiri anapigia mziki wananchi waliojaa uwanja wa Karume, majirani tunateseka sana:mad:
 
Mazoea mabaya, lazima kuna sheria au kanuni za manispaa au leseni ambazo zinatoa maelekezo na hivyo inawezekana hiyo ndiyo sheria ila ilikua tu haifutwi. Hata hivyo sheria si msahafu inaweza ikarekebishwa ikawa tofauti na hilo tangazo lkn pia bila kuathiri mambo mengine. Mziki wa baadhi ya bar ni kero kwa wanaoishi jirani na bar hizo, hivyo ni lazima kiwango cha sauti kithibitiwe.
 
Hii tutaipinga mahakamani Kwan inaingilia uhuru wetu. Ina maana hâta baa za mahoteli zitafuata utaretibu Huu?
 
Hivi kwani kunywa pombe ni lazima? pombe imegeuka ibada? tuacheni ubishi usio na maana. Ni juzi mmeambiwa 71% hamfanyi kazi inavyostahili kwasababu ya kupenda starehe mno ila bado hata hamuoni tofauti. Ukitaka kunywa nunua unywee kwako.
 
Makanisa ya kiloloke nayo vipi? hao waislamu vipi nao na vipaza sauti na mahaburi ya kunitishana sijui kiama sijui kifo sijui sanda kiukweli kelele ktk nyumba za ibada na bar wathibiti tu
 
Back
Top Bottom