KINGWENDU: Nataka kuwa kama Mr Bean | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KINGWENDU: Nataka kuwa kama Mr Bean

Discussion in 'Entertainment' started by kilimasera, May 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  UKITAJA wasanii wakali wa filamu na hasa vichekesho hapa nchini, huwezi kumwacha Kingwendu .
  Kingwendu ambaye jina lake halisi ni Rashid Mwinyishehe Mzange, anakipaji cha kumfanya mtu anayemwangalia kucheka kabla hajatamka neno lolote. Kicheko kitaongezeka zaidi akianza kuzungumza vibwagizo vyake vya kuchekesha kama vile: “Heluu”.
  Kingwendu ameshiriki katika kuingiza filamu nyingi za vichekesho zinazoendelea kutamba nchini kama vile ‘Inye’, vituko show na michezo mingine mingi ya kuchekesha.

  Kama ilivyo kwa wasanii wengi ambao huvutiwi na kazi za wasanii wenzao, Kingwendu anasema anatarajia kiwango chake cha uchekeshaji kitafikia cha mchekeshaji nguli anayetikisa dunia, Mr Bean.

  Kingwendu anasema anataka kufuata nyayo za Mr Bean katika uingizaji wake, ili kuwafurahisha watazamaji wake ikiwa ni pamoja na kumfanya mtu aliyeko kwenye majonzi au msiba kusahau machungu yake.

  Kingwendu anasema, mbali na kuvutiwa na kazi za Mr Bean na kutamani kufikia kiwango chake, kuna wasanii hata hapa nchini ambao wanamvutia akiwamo, Mzee Majuto.

  “Mzee King Majuto anajituma sana awapo jukwaani, anaweza kulitawala jukwaa vilivyo. Nadhan hata wewe unalifahamu hilo, kwa sababu hajaanza leo kuigiza vichekesho. Yaani yule jamaa ni muigizaji wa muda mrefu katika fani hii na ana mashabiki wengi,” anasema Kingwendu.

  Mkali huyo wa vichekesho mwenye mitindo ya aina yake awapo kazini, anasema pamoja na wasanii wengi wa bongo kufahamika na wengi kutokana na kazi zao hawanufaiki na kazi zao.

  “Ukiona baadhi ya wasanii wenzetu wanatembelea magari yao binafsi, lakini wengi wetu bado tunakimbizana kwenye daladala kutokana na wafadhili wao kutowasaidia,” anasema.

  Anawataja wasanii wenye ufadhili wenye mafanikio mazuri hapa nchini kuwa ni pamoja wa kundi la Ze Comedy ambao wanatembelea magari yao na wana uhakika wa kujenga nyumba kutokana na kipato chao.
  Kuhusu mipango yake kwa mwaka huu, Kingwendu anasema hadi sasa ameshaandaa filamu tatu ambazo bado hazijaingia sokoni.

  Amezitaja filamu hizo kuwa ni ‘Mwanamke kazi’, ‘Mwanaume kazi’, ‘Mkataa pema’ na ‘Govinda.

  “Tena hii ya Govinda ndio kiboko kwani sitaki hata kuelezea inahusu nini, lakini mashabiki wangu wakae mkao wa kula. Ebwanaee si mchezo, ni nomaa,” anasema.

  Msanii huyo ambaye anachekesha muda wote, anasema katika filamu zake amewashirikisha wasnii wakongwe kama Mzee Majuto, Senga, Muhogo Mchungu na Pembe.

  Akizunfumzia kuhusu wasanii, aliwataka kuacha malumbano badala yake watafute njia ya kufanikiwa kimaisha badala ya kuendeleza majungu, kuonekana wivu na kupigana vita .

  “Unajua, majungu ni sumu ya maendeleo kabisa katika tasnia hii ya sanaa yetu hivyo tukiendekeza majungu inakula kwetu,” anasema Kingwendu.

  Kingwendu ameoa na ni baba wa watoto watatu Maua, (10), Khadija (4) na Mwamvita (3). Mkewe ni mtoto wa aliyekuwa mchora katuni maarufu za Chakubanga. Pia amejenga nyumba kutokana na kazi ya usanii.
  

  Kingwendu alianza kuwika katika fani ya uigizaji mwaka 2002 akiwa na mkali mwingine, Bambo na baadaye wote waliamua kuimba na wamekuwa wakichanganya muziki wa kizazi kipya na ya asili, kama vile 'Mdundiko' na 'Mchiriku'.
   
 2. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  labda akiacha Gongo
   
 3. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ebu upload picha yake hapa tumwone huyo jamaa ambaye anachekesha kabla hata hajatamka neno.
   
 4. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Tatizo wanajua sawa uhuwezi kuwa kimataifa kama hufanyi juhudi kuwa kimataifa,so watavuma hapahapa mpaka mwisho,wanavipaji ila hawana uweledi(shule ndogo)
   
 5. MAMESHO

  MAMESHO Senior Member

  #5
  Feb 17, 2014
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  you cant be someone else. king'wendu atakuwa king'wendu tu. kutamani mafanikio ya Mr Bean bila kutamani kazi anazofanya kufika alipo ni kama ndoto za mvuta bhange aliyeko tandika akaona yuko marekani
   
 6. GENTAMYCINE

  GENTAMYCINE JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2014
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 23,005
  Likes Received: 22,567
  Trophy Points: 280
  Nikiwa Kama Mpenda Vichekesho Ninampenda na Namkubali Sana Kingwendu na Namtakia Mafanikio ktk Kazi Zake za Usanii wa Vichekesho. Jamaa Anajua.....................!
   
 7. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2014
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,804
  Trophy Points: 280
  All the best tunataka vitendo na si maneno
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2014
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo ni kweli kabisa, kuna Yule mwingine alikuwa anabeba rungu kwenye michezo naye anafanya vyema
   
 9. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2014
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,351
  Likes Received: 2,693
  Trophy Points: 280
  Ni miaka miwili na ushee sasa imepita nahisi muota ndoto kaamka na ndoto imekatika...
   
 10. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2014
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,351
  Likes Received: 2,693
  Trophy Points: 280
  Anaitwa Pembe...
   
 11. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2014
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Yes darling thanks..... Huwa nacheka sana na kuna yule mwingine huwa ana kigugumizi anavaa bwanga he he heee huwa wanaongozana na Pembe.
   
 12. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2014
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,351
  Likes Received: 2,693
  Trophy Points: 280
  Hahah!!!

  Yes darling huwa wanachekesha sana hawa jamaa...huyo uliyemtaja nahisi wamzungumzia Mzee Senga
   
Loading...