Kingunge ulisema Kikwete alikuwa na jina la mgombea rais mfukoni, vipi Mbowe humsemi?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Mzee Kingunge alizunguka akiimba kwenye majukwaa kuwa majina ya wagombea Uraisi Mwenyekiti wa CCM KIKWETE alikuwa nayo mfukoni mwake wengine walikuwa hawajui.Mzee akachukia hadi akahama chama.Wana CHADEMA kama kawaida wakaiponda sana CCM kwa kuwa mwenyekiti ana majina mfukoni.

Sasa majina ya katibu mkuu CHADEMA tunaambiwa Mbowe anayo mfukoni Kingunge mbona haongelei hilo? Muulizeni mzee mbona uko Kimya?.

Ajabu hata wana CHADEMA wenyewe wako kimya.Hata akina SUMAYE waliokuwa wakilaani Kikwete kuwa alikuwa na majina mfukoni nao kimya kulikoni?

Majina akiwa nayo mfukoni mwenyekiti wa CCM ni kosa lakini mwenyekiti wa CHADEMA akiwa nayo mfukoni ni sawa!!!!!!!!!! Mnachekesha sana CHADEMA

Kingunge kwenye hili suala la kisiasa karuka mkojo kakanyaga mavi
 
Ungekuwa unajua utaratibu unaotumika kumpata mgombea urais na katibu mkuu wa chama, wala usingehangaika kuanzisha thread yenye maneno mengi hivyo. Kwa ufupi, mgombea urais anapendekezwa (anateuliwa) na chama, wakati katibu mkuu anaajiriwa na chama.
Huoni aibu wenye mlengo wako wote wapo kimya hawaji kukusapoti? Wanajua umewaaibisha kwa bandiko hili linaloonyesha kichwani hakuna kitu
 
Hiyo ajira mbona mie sikuiona magazetini ili nami niombe?
 
Mkuu @yehodaya,jipe muda wa kusoma hata katiba za vyama. Katiba ya chama cha akina Mbowe inaruhusu Mwenyekiti kumteua Katibu Mkuu kama ilivyo yetu ya CCM. Kwa ulivyoropoka,aibu naona mimi!

Mzee Tupatupa
Basi katiba za vyama vyenu zote mbaya ( hazina uwazi na si za kidemokrasia)
 
Ni vema kabla hujapost kitu jihakikishe uhakika wake.. Mwenyew unasema UMESIKIA then unakurupukia if ...
Kaa utulie
 
MLETA MADA UMEJIVUA NGUO UMEONYESHA WEWE NI ZIRO KWENYE KUSOMA NENDA KATAFUTE KATIBA YA BORA KABISA YA CHADEMA UPITIE
 
Basi katiba za vyama vyenu zote mbaya ( hazina uwazi na si za kidemokrasia)
Ni mfumo unaofanana karibu sekta zote sasa kuwa Katibu Mkuu ni mwajiriwa ili aweze kuwajibika kwa mazuri na mabaya ya utendaji wake. Hebu angalia TFF ilivyopokea maagizo ya FIFA kuwa vilabu vyote wanachama wa shirikisho viwe na katiba inayomtaja katibu mkuu kama mwajiriwa, na ndio maana siku hizi uchaguzi wa vilabu huwa hauhusu nafasi ya katibu mkuu. Kama unafuatilia soka la bongo, juzi juzi hapa mwenyekiti wa Yanga alimfukuza katibu mkuu wake kwa alichokiita 'utendaji usioridhisha'. Sasa kama katibu mkuu angekuwa amechaguliwa na mkutano, hata akiboronga si rahisi mtu mmoja kumfukuza, hadi mkutano tena ndio umfukuze. Mweka hazina pia anaangukia katika kundi la waajiriwa
 
naendelea kusisitiza semina zitolewe zaid kwa hawa vijana wapya wa lumumba buku7 maana wanazidi kuhadhirika,lizaboni fikisha hizi habari maana humu wana pambana na umma wenye fikra huru na wasio na maslahi hata chembe.
 
Mkuu @yehodaya,jipe muda wa kusoma hata katiba za vyama. Katiba ya chama cha akina Mbowe inaruhusu Mwenyekiti kumteua Katibu Mkuu kama ilivyo yetu ya CCM. Kwa ulivyoropoka,aibu naona mimi!
Mzee Tupa tupa mnyang'anye ID huyo ametutia aibu wengi.

Mzee Tupatupa
 
Wewe mleta uzi Ccm wamekuokota wapi? Hawajakupa mafunzo? Next time kabla huja post thread humu mkabidhi kwanza mkuu wako wa kitengo aifanyie editing, otherwise wakupeleke kwenye kitengo cha kuuza kofia na t-shirts za chama Lumumba.
 
naendelea kusisitiza semina zitolewe zaid kwa hawa vijana wapya wa lumumba buku7 maana wanazidi kuhadhirika,lizaboni fikisha hizi habari maana humu wana pambana na umma wenye fikra huru na wasio na maslahi hata chembe.
TataMadiba na Lizaboni mnaitwa huku muwape semina vijana, wanaaibisha chama letu
 
Mtoa hoja ni mbumbu kweli kweli kweli! Nani aliwachagua Yusuf Makamba, Mukama na sana Kinana kuwa Makatibu wakuu wa CCM. Hata Makamu Mwenyekiti wa CCM anateuliwa na Mwenyekiti.
 
Mzee Kingunge alizunguka akiimba kwenye majukwaa kuwa majina ya wagombea Uraisi Mwenyekiti wa CCM KIKWETE alikuwa nayo mfukoni mwake wengine walikuwa hawajui.Mzee akachukia hadi akahama chama.Wana CHADEMA kama kawaida wakaiponda sana CCM kwa kuwa mwenyekiti ana majina mfukoni.

Sasa majina ya katibu mkuu CHADEMA tunaambiwa Mbowe anayo mfukoni Kingunge mbona haongelei hilo? Muulizeni mzee mbona uko Kimya?.

Ajabu hata wana CHADEMA wenyewe wako kimya.Hata akina SUMAYE waliokuwa wakilaani Kikwete kuwa alikuwa na majina mfukoni nao kimya kulikoni?

Majina akiwa nayo mfukoni mwenyekiti wa CCM ni kosa lakini mwenyekiti wa CHADEMA akiwa nayo mfukoni ni sawa!!!!!!!!!! Mnachekesha sana CHADEMA

Kingunge kwenye hili suala la kisiasa karuka mkojo kakanyaga mavi
Pilipili iliyoko shamba inakuwashia nini mjini?
 
MLETA MADA UMEJIVUA NGUO UMEONYESHA WEWE NI ZIRO KWENYE KUSOMA NENDA KATAFUTE KATIBA YA BORA KABISA YA CHADEMA UPITIE
Haki ya nani kweli hawa watetezi wa ccm ni ziro brain kabisa. Eti huyo ndio kalala anafikiri kuja kuanzisha Uzi mbumbumbu kama huu.
Ina mpaka mzee wao Tupatupa anasema anaona aibu jinsi huyu binti alivyojichoza bila kuelewa.
Nape angekuwa makini angemfukuza kwenye group 46. Na hawa ndio wanaombewa ajira kwa Magu na Mwenyekiti wao.
 
MLETA MADA UMEJIVUA NGUO UMEONYESHA WEWE NI ZIRO KWENYE KUSOMA NENDA KATAFUTE KATIBA YA BORA KABISA YA CHADEMA UPITIE
anakuja na katibu bora kabisa sijui nani alimfanyia usaili, kwanini aanze kujihami si awaachie wajumbe wamwone bora?
 
Back
Top Bottom