Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,011
- 74,659
Lazima tukubali Mzee Kingunge anazijua sana siasa za nchi hii kwani ameshiriki kwa kipindi kirefu sana. Almost 61 years yupo katika ulingo huo wa siasa katika nafasi nyingi. Tena sio katika ushiriki ule wa "Ndio mzee" bali pia wa misukosuko ndani ya chama chake na serikali kama alivyoeleza mwenyewe jana.
Kwa maana hiyo TANU na CCM anaijua zaidi kuliko Kikwete, Kinana na wengine wengi wakiwamo wakina Msekwa na Warioba. Lakini katamka wazi kuwa CCM ya sasa sio ile iliyokuwa na misingi yake ya awali bali hii imebinafsishwa na hajui kwa manufaa ya nani (ingawa nadhani anajua).
Kauli mbiu yake ni kuwa CCM imekuwa OBSOLUTELY POWER CORRUPTS na haiwezi tena kuongoza, ni sawa na mtu anayepanda mlima na kisha akaishiwa pumzi inambidi ashuke tuu. Maneno hayo kwa wale wanaoendelea kuiunga mkono CCM wameyaelewa? Mkongwe kasema chama chao ndio kimefikia mwisho iweje nyie tena wengi wamezaliwa kikiwepo wao wasimuelewe huyu mzee?
ONDOKENI HUKO SASA, ASIYESIKIA LA MKUU ........!