jogoolashamba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 348
- 71
Kauli ya Mh Rais John Pombe Joseph Magufuli kuwa atawalinda Marais wastaafu dhidi ya mashitaka inatia woga. Mamlaka ya Rais wa sasa asiyeshtakika yana uhuru mkubwa wa mwenye kuwa nayo kuibia nchi na hata kufanya vituko bila shaka ya kuulizwa. Mamlaka ya namna hiyo yanatuletea ile dhana haswa ya Miungu-Watu. JPM anayo nafasi nzuri ya kuingiza nchi katka utaratibu wa utawala wenye kuheshimu sheria na rasilimali za Taifa. Akisikia kauli za "Rais mstaafu ashitakiwe" zikitokea uraiani ajue kuna makubwa tunayoyaona na kuyajua.
AKIONA ATALAUMIWA NA WALIOMTANGULIA BASI AITISHE KURA YA MAONI KUHUSU HILI.
Wastaafu hawa wana nguvu zinazopindukia hata baada ya kuondoka Ikulu. Mifano ni mingi lakini sikia huu: Mzee Mwinyi yeye mwenyewe alikamata mkusanyaji kodi wa majumba yake ya kupangisha nakumwekea Hakimu Kisutu, hayakuwa madai, Mwinyi aliagiza mtuhumiwa wake afunguliwe jinai na bila upelelezi wa Polisi jinai ikaendeshwa kwa ushahidi wa Mzee Mwinyi mwenyewe. Mimi hapo ndipo nikajua kumbe Mzee Mwinyi ana majumba ya kupangisha, aliyajenga lini?
Kutowadhibiti hawa kupitia katiba baadaye kutajatuzalishia Majambazi tusiyoyaweza kwa sababu ya kinga hizo. Hakuna aliyekwishaufikia uadilifu wa Mwalimu hivyo kinga ziondolewe ili Marais waongozwe na Katiba, siyo wajiongoze wenyewe kama ilivyo sasa.