King Majuto Adaiwa Kumtokea Mkewe

King Majuto Adaiwa Kumtokea Mkewe

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
mzee-majuto.jpg

DAR ES SALAAM:
Baada ya maneno mengi huku ndugu wa aliyekuwa mumewe, Amri Athuman ‘King Majuto’ wakidaiwa kumnyima huduma muhimu kama chakula, mjane wa mzee huyo aliyekuwa kinara wa vichekesho Bongo, Aisha Yusuf anadaiwa kutokewa na mzee huyo kwani hafurahishwi na vitendo vinavyoendelea.

Kufuatia madai hayo huku mama huyo akiwa ameondoka Tanga na kurejea kwa wazazi wake jijini Dar, gazeti hili lilimtafuta Aisha ambaye katika mahojiano maalum alielezea hali hiyo;

Risasi Jumamosi: Habari mama, unaendeleaje?

Aisha: Sijambo, naendeelea vizuri.

Risasi Jumamosi: Kuna tofauti gani ya kimaisha tangu Mzee Majuto aondoke?

majutos.jpg

Aisha: Lazima kuwe na utofauti ingawa ninamshukuru Mungu mimi sijambo.

Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa Mzee Majuto amekutokea hivi karibuni baada ya matatizo yako, je, unalizungumziaje hilo?

Aisha: Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwa sababu mimi nilikuwa karibu naye. Kwa yeyote anayefiwa, atakutana na hali hii ingawa ni mapema mno kuliongelea.

Risasi Jumamosi: Kwa nini unasema ni mapema mno? Je, hakuna chochote amekuambia katika kukutokea huko?

Aisha: Sina la kusema zaidi ya hapo kwani hata watoto bado yupo machoni mwao wanamuona, mara nyingi hata kiimani, kinachoondoka ni kiwiliwili tu, lakini roho bado inakuwepo, kwa hiyo kusema Majuto hajanitokea siwezi kwani namuona wakati wote.

Chanzo:Global Publishers
 
Huuyo mkewe alikua amekula cha arusha au cha kigoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya magazeti saazingine yanapenda kuwalisha watu maneno.
Hiyo interview, kuna sehemu huyo mjane kasema amemuota marehemu, au wao ndiyo wamemueleza kuwa wamesikia ameota?
Hakuna kitu ninachochoka sana siku hizi kama uandishi huu horijojo.
Unakuta kichwa cha habari ni tofauti kabisa na kiwiliwili chake!
Wapo hawa wa magazeti pamoja na blogers!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata sisi huku JF katutokea mara mbili. Kama unabisha angalia kwenye thread utamuona.
 
Back
Top Bottom