lendila
JF-Expert Member
- Sep 26, 2012
- 5,806
- 4,370
Bw Hakainde Hichilema, ni kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia
Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, alizuia msafara wa Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu mwishoni mwa juma.
Hii ni kulingana na taarifa iliyotolewa kutoka kwa msemaji wa rais.
- Upinzani unaongoza kwa kura za urais Zambia
- Kinara wa upinzani nchini Zambia azuia msafara wa Rais
- Waliofanya ghasia wakamatwa Zambia
Haijafahamika iwapo hatua hiyo inatokana na kisa cha mara kwa mara cha kuvamia nyumba ya Bw Hichilema iliyoko katika mji mkuu, Lusaka.
Kwa sasa kiongozi huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi.
Ameliambia gazeti moja la Afrika Kusini- Daily Maverick kwamba, rais anataka kumuuwa.
Bw Hichilema, alipewa dhamana mwezi Oktoba mwaka jana, baada ya kushtakiwa kwa kosa la fitna, hatua ambayo kikosi chake kilisema ni mbinu za chama tawala za kutaka kumnyamazisha.
Chanzo: BBC Swahili